Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Njombe, Mrisho Mwisimba (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa Sylvester Mpanduji aliyetembelea banda la NSSF katika maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yanayoendelea mkoani Njombe. SIDO kwa kushirikiana na NSSF, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC), VETA na benki ya Azania kwa pamoja wanaratibu mpango wa kuendeleza viwanda vidogo na vya kati (SANVN VIWANDA SCHEME) ambapo tayari NSSF imeshatoa bilioni 5, huku SIDO na VETA wanahusika na utambuzi wa wajasiriamali, NEEC kazi yake ni kuratibu mpango huo na benki ya Azania inahusika kutoa mikopo hiyo.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Njombe, Mrisho Mwisimba(kulia) akimpa maelezo Kaimu Katibu Mkuu wa Wiraza ya Kilimo, Dkt. Honest Kessy (Kushoto)alipotembelea maonesho ya Nane ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mji Mwema mkoani Njombe.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Njombe, Mrisho Mwisimba akizungumza katika maonesho ya Nane ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mji Mwema mkoani Njombe, ambapo amewahimiza wananchi kujiunga na Shirika hilo ili wanufaike na mafao mbalimbali yanayotolewa na NSSF
Social Plugin