Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Salome Makamba (kulia) akiwasalimia wananchi katika Mtaa wa Kalonga Kata ya Ngokolo wakati Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo,Emmanuel Ntobi (kushoto) akinadi sera za CHADEMA na kuomba kura kwa wananchi.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Salome Makamba 'Ng'wana O Shimba' ameendelea kuchanja mbuga katika mitaa mbalimbali Mjini Shinyanga ambapo leo amefanya Mkutano wa Kampeni katika Mtaa wa Kalonga Kata ya Ngokolo.
Salome Makamba aliwasili eneo la Mkutano Majira ya 11 na dakika 40 jioni wakati Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo,Emmanuel Ntobi akiwa jukwaani akiendelea kunadi sera za CHADEMA na kuomba ridhaa wananchi wamchague kuwa Diwani wa Kata hiyo pamoja na wagombea wengine wa CHADEMA akiwemo Salome Makamba (Ubunge) na Tundu Lissu (Urais Tanzania).
Mara baada ya Salome Makamba kuwasili eneo la Mkutano wa Kampeni na kupanda jukwaani, akina mama waliokuwa wakifuatilia sera za CHADEMA walivua khanga,mitandio,vitenge na vikoi walivyokuwa wamevaa kisha kuvitandika chini kuanzia eneo la jukwaa hadi sehemu walipokuwa wamekaa viongozi wa CHADEMA ili pindi atakaposhuka jukwaani akanyage juu ya nguo hizo ikiwa ni ishara ya kumpa heshima kubwa kama Mwanamke Shujaa/Shupavu na imara aliyesimama kuwatetea na kuwaletea maendeleo wananchi wa Shinyanga.
Akinadi sera za CHADEMA na kuomba kura, Salome Makamba alisema amedhamiria kuwaletea maendeleo wananchi wa Shinyanga akijinasibu kuwa ana uwezo mkubwa wa kusimamia Jimbo la Shinyanga Mjini lakini pia ana uwezo mkubwa wa kuwatetea wananchi wa Shinyanga.
“CHADEMA tumeshamaliza shughuli ya Kampeni. Shughuli ya Kampeni tumeshaimaliza,kinachotakiwa ni nyinyi wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura Oktoba 28,2020. Chagueni wagombea wa CHADEMA,Pigeni kura za kutosha kunichagua kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,kumchagua Emmanuel Ntobi kuwa diwani wa Ngokolo na Tundu Lissu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”,alisema Salome.
“CHADEMA tunataka Jimbo la Shinyanga lifanane na Shinyanga Mjini, Hii ni Shy Town lakini bado haijafanana kuwa mjini haswa. Nichagueni niwe Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ili kubadilisha Mji huu kwani nimedhamiria kuleta mabadiliko makubwa Shinyanga”,aliongeza Salome.
Kwa upande wake, Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo, Emmanuel Ntobi alisema Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28,2020 siyo wa kufanyia masihara hivyo kuwaomba wananchi wasifanye makosa bali wachague wagombea wa CHADEMA.
Ntobi alivitaja baadhi ya vipaumbele vyake katika kata ya Ngokolo kuwa ni kuboresha sekta ya afya kwa kujenga kituo cha afya na kujenga soko la kisasa Ngokolo Mitumbani litakalowawezesha wafanyabiashara kufanya biashara hadi nyakati za usiku.
Vipaumbele vingine ni katika sekta ya elimu ambapo Ntobi ameahidi kuanzisha ujenzi wa shule ya Kidato cha tano na sita,kuanzisha SACCOS ya kata,kusimamia upatikanaji wa mikopo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu,kuboresha michezo na kujenga maghuba ya taka.
“Ndugu zangu wananchi wa kata ya Ngokolo naombeni mtuchague ili kuwaletea maendeleo. Tuchagueni ili tukatatue pia changamoto ya muda mrefu ya bili kubwa za maji”, aliongeza Ntobi.
Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA, Emmanuel Ntobi akiwahutubia na kuwaomba kura wananchi wa mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo wamchague kuwa diwani wa kata hiyo leo Jumapili Oktoba 11,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA, Emmanuel Ntobi akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo
Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA, Emmanuel Ntobi ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga akiwaomba wananchi kuchagua wagombea CHADEMA kuanzia ngazi ya Udiwani,Ubunge na Urais.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Salome Makamba akimuombea kura kwa wananchi Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo,Emmanuel Ntobi (kushoto) lakini pia kujiombea kura yeye mwenyewe achaguliwe kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Salome Makamba akiwahutubia wananchi katika Mtaa wa Kalonga Kata ya Ngokolo kabla wanawake waliokuwa katika eneo la mkutano wa Kampeni hawajavua khanga,vitenge,vikoi na mitandio waliyokuwa wamevaa na kutandika chini ili Mgombea Ubunge Salome akanyage baada ya kumaliza kuomba kura kwa wananchi ikiwa ni Ishara ya kumpa heshima ya pekee kama Mwanamke Shupavu na Imara.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Salome Makamba akiwahutubia wananchi katika Mtaa wa Kalonga Kata ya Ngokolo huku wanawake waliokuwa katika eneo la mkutano wa Kampeni wakitandika chini khanga,vitenge,vikoi na mitandio waliyokuwa wamevaa ili Mgombea Ubunge Salome akanyage baada ya kumaliza kuomba kura kwa wananchi ikiwa ni Ishara ya kumpa heshima ya pekee kama Mwanamke Shupavu na Imara.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Salome Makamba akiwahutubia wananchi katika Mtaa wa Kalonga Kata ya Ngokolo huku wanawake waliokuwa katika eneo la mkutano wa Kampeni wakitandika chini khanga,vitenge na vikoi walivyokuwa wamevaa ili Mgombea Ubunge Salome akanyage baada ya kumaliza kuomba kura kwa wananchi ikiwa ni Ishara ya kumpa heshima ya pekee kama Mwanamke Shupavu na Imara.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Salome Makamba akiwahutubia wananchi katika Mtaa wa Kalonga Kata ya Ngokolo

Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo kupitia CHADEMA, Emmanuel Ntobi ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga akimuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba (kushoto).

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba (kushoto) akipokea michango mbalimbali ya wanachama wa CHADEMA na wananchi wakichangia CHADEMA
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba (katikati) akipita kwenye khanga,vitenge,mitandio na vikoi vilivyotandikwa chini na akina mama wa mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo ikiwa ni heshima waliyompatia kama Mgombea Mwanamke shupavu na imara.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba (katikati) akipita kwenye Kanga,vitenge,mitandio na vikoi vilivyotandikwa chini na akina mama wa mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo ikiwa ni heshima waliyompatia kama Mgombea Mwanamke shupavu na imara.

Kada wa CHADEMA Seleman Khalid akiwaombea kura wagombea wa CHADEMA
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini, Samson Ng'wagi akiwaombea kura wagombea wa CHADEMA
Wananchi wa mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo Jimbo la Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa kampeni CHADEMA.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin