WASAIDIZI WA KISHERIA WAONYWA KUSULUHISHA KESI ZA MAKOSA YA JINAI ,MATUKIO YA UKATILI WA KIJINSIA


Wakili Neema Ahmed



Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’ wametakiwa kuepuka kufanya usuluhishi wala upatanishi panatokea matendo ya ukatili wa kijinsia ambayo ni makosa ya jinai badala yake wapeleke mashauri ya jinai kwenye ngazi zinazostahiki ikiwemo Dawati la jinsia na watoto,polisi au kwa walinzi wa amani wa maeneo husika.


Rai hiyo imetolewa leo Jumapili Oktoba 4,2020 Mjini Shinyanga na Wakili Neema Ahmed wakati wa mafunzo ya siku tatu yaliyoanza leo kwa Wasaidizi wa Kisheria 27 kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Kishapu yaliyoandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na UNFPA na KOICA yakiwa na lengo la kukuza uelewa wao kwenye masuala ya kijinsia na namna gani watashiriki katika harakati za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye jamii.

“Msaidizi wa Kisheria ukiletewa Mashauri ya jinai kama vile ya vipigo,ubakaji,ulawiti,mashambulio ya aibu,tafadhali usifanye usuluhishi wala upatanishi bali yapeleke kwenye ngazi za ili hatua zichukuliwe dhidi ya wahusika wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake”,alisema Neema.

“Makosa ya jinai hayasuluhishwi. Msaidizi wa Kisheria unasuluhisha jinai kama nani?, mtu anasema amepigwa unaanza kufanya usuluhishi ili iweje? Kama ni kosa la jinai unatakiwa kwenda polisi au kwa afisa mtendaji wa kata au kijiji ili wao wawasiliane na polisi kwa ajili ya hatua zaidi. Jukumu lako ni kuwaeleza waende kwenye maeneo husika”,aliongeza Neema.

Mwanasheria huyo aliwaasa wasaidizi wa kisheria pale wanapopokea kesi za jinai wasikubali kusuluhisha,wawambie wahusika waende kwenye dawati la jinsia au kwa walinzi wa amani wakiwemo maafisa watendaji kata na vijiji huku akiwasisitiza kuwa hata upelelezi wa kesi za jinai siyo sehemu ya majukumu yao.

Nao Wasaidizi wa kisheria walioshiriki katika mafunzo hayo wameyataja mashauri/kesi zinazoongoza kuwafikia ni zile zinazohusu masuala ya ardhi,mirathi, migogoro ya ndoa na matunzo ya watoto.

Hata hivyo walizitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia kuogopa kutoa ushirikiano,waathirika kuwa wasiri hawataki kuongea yanayowasibu lakini pia baadhi ya Wasaidizi wa kisheria wanapata vitisho wanapofuatilia baadhi ya kesi.
Mwezeshaji/Mwanasheria Neema Ahmed akizungumza wakati wa mafunzo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia kwa wasaidizi wa kisheria ambapo aliwasititiza kuepuka kufanya usuluhishi wala upatanishi kwenye kesi zinazohusu makosa ya jinai.
Mwezeshaji/Mwanasheria Neema Ahmed akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu yaliyoanza leo kwa Wasaidizi wa Kisheria 27 kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Kishapu yaliyoandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na UNFPA na KOICA yakiratibiwa na shirika la PACESHI yakiwa na lengo la kukuza uelewa wao kwenye masuala ya kijinsia na namna gani watashiriki katika harakati za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye jamii.
Mwanasheria  Jenesia Mavere ambaye ni miongoni mwa wawezeshaji akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu yaliyoanza leo kwa Wasaidizi wa Kisheria 27 kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Kishapu yaliyoandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na UNFPA na KOICA yakiratibiwa na shirika la PACESHI yakiwa na lengo la kukuza uelewa wao kwenye masuala ya kijinsia na namna gani watashiriki katika harakati za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye jamii.
Meneja Mradi wa Huduma ya Msaada wa Kisheria kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) John Shija kutoka Shirika la PACESHI la Shinyanga mjini  akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya Ushetu na Kishapu yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),UNFPA na KOICA na kuratibiwa na PACESHI kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Meneja Mradi wa Huduma ya Msaada wa Kisheria kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) John Shija kutoka Shirika la PACESHI la Shinyanga mjini  akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya Ushetu na Kishapu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.
Msajili Msaidizi wa Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria halmashauri ya wilaya ya Kishapu Efrem Kilango akizungumza katika mafunzo hayo ambapo alisema majukumu ya Wasaidizi wa kisheria pamoja na kusaidia jamii za maeneo yao kuhusu masuala ya kisheria hususani ukatili wa kijinsia na pale Msaidizi wa Kisheria anapoona shauri limeshindikana atoea rufaa kwenda ngazi za juu kama ofisi za maafisa watendaji wa kata,vijiji, polisi au mahakamani.
Msajili Msaidizi wa Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria halmashauri ya wilaya ya Kishapu Efrem Kilango akizungumza katika mafunzo hayo.
Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya Ushetu na Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia
Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya Ushetu na Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post