Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI YA TPB SHINYANGA YAENDELEA KUSHEREHEKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA ....YAANIKA FURSA KWA WANANCHI


Benki ya TPB tawi la Shinyanga inaendelea kusherehekea Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Jumatatu Oktoba 5,2020 ambapo inawaleta pamoja wateja wao wakipata fursa ya kuonana nao, kupata maoni yao kuhusu huduma wanayoipata, kuwapatia zawadi mbalimbali na kuwashukuru kwa kuwa wateja na sehemu ya Benki ya TPB.


Akizungumza mapema leo Jumanne Oktoba 6,2020 Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Shinyanga Julius Mataso amewaomba wateja wa TPB Bank na wananchi ambao bado hawajajiunga na benki hiyo kuchangamkia fursa zilizopo katika Benki hiyo ikiwemo Huduma ya Mikopo kwa Wastaafu,Wajasiriamali, Watumishi na Wakulima.

Mataso amezitaja Huduma zingine zinazopatikana TPB Bank kuwa ni pamoja na Mikopo ya Nyumba na Bima za aina zote ikiwemo ya Magari, Akaunti ya Muda Maalum (miaka miwili) kwa ajili ya Uwekezaji ambayo Riba yake ni asilimia 9 kwa mwaka.

Mataso amesema Huduma nyingine ni Kutuma na Kupokea Fedha nje na ndani ya nchi kupitia Western Union.

Aidha amesema Benki ya TPB itaendelea kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu kwa wateja wote huku akiwakaribisha wananchi ambao hawajafungua Akaunti wafike katika Benki ya TPB ili kupata huduma bora.

Wafanyakazi wa Benki ya TPB tawi la Shinyanga wakiwa ndani ya Benki kabla ya kuanza kuhudumia wateja leo asubuhi Jumanne Oktoba 6,2020 . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Muonekano wa Keki Maalum zilizoandaliwa na Benki ya TPB tawi la Shinyanga kwa ajili ya Wateja wa Benki ya TPB.


Wafanyakazi wa kiume wa Benki ya TPB wakiwa wameshikilia Keki Maalum kwa ajili ya Wateja wa Benki ya TPB leo Jumanne Oktoba 6,2020. Kushoto ni Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Shinyanga Julius Mataso 
Wafanyakazi wa Benki ya TPB wakiwa wameshikilia Keki Maalum kwa ajili ya Wateja wa Benki ya TPB leo Jumanne Oktoba 6,2020
Wafanyakazi wa kike wa Benki ya TPB wakiwa wameshikilia Keki Maalum kwa ajili ya Wateja wa Benki ya TPB leo Jumanne Oktoba 6,2020
Wafanyakazi wa Benki ya TPB wakiwa wameshikilia Keki Maalum kwa ajili ya Wateja wa Benki ya TPB leo Jumanne Oktoba 6,2020
Wafanyakazi wa Benki ya TPB tawi la Shinyanga wakiwa ndani ya Benki kabla ya kuanza kuhudumia wateja leo asubuhi Jumanne Oktoba 6,2020
Wafanyakazi wa Benki ya TPB  wakipiga picha ndani ya Benki kabla ya kuanza kuhudumia wateja leo asubuhi Jumanne Oktoba 6,2020
Wafanyakazi wa Benki ya TPB wakipiga picha  ndani ya Benki kabla ya kuanza kuhudumia wateja leo asubuhi Jumanne Oktoba 6,2020
Wafanyakazi wa Benki ya TPB wakipiga picha  ndani ya Benki kabla ya kuanza kuhudumia wateja leo asubuhi Jumanne Oktoba 6,2020
Wafanyakazi wa Benki ya TPB wakipiga picha  nje ya Benki kabla ya kuanza kuhudumia wateja leo asubuhi Jumanne Oktoba 6,2020
Wafanyakazi wa Benki ya TPB wakipiga picha  nje ya Benki kabla ya kuanza kuhudumia wateja leo asubuhi Jumanne Oktoba 6,2020.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com