TIGO WAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2020




Mwangaza Matotola,Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa Wateja Tigo akizindua wiki ya huduma kwa wateja
Dora Mzinga, mwakilishi wa watoa huduma kwa wateja, akiongea kuelezea jinsi watoa huduma wa Tigo walivyojipanga kwa wiki hii


  • Kutoa tuzo kwa wafanyakazi wake wa kitengo cha huduma kwa wateja
Dar es Salaam. 5 Octoba 2020. Kampuni ya mawasiliano inayoongoza kwa kutoa huduma za kidigitali nchini, Tigo Tanzania, leo inaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kutambua na kusherehekea huduma nzuri zinazotolewa na wafanyakazi wake wa kitengo cha huduma kwa wateja ambao siku zote wapo mstali wa mbele kuipeperusha bendera ya kampuni hiyo kwa wateja kupitia njia mbalimbali za mawasiliano.
Sherehe hizi za wiki nzima zitaenda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni ‘Dream Team’. Kauli mbiu hii inaakisi umuhimu wa kufanya kazi kama timu moja katika kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa za ubora wa hali ya juu kwa wateja wote. Hii pia imelenga kuwapongeza wafanyakazi wa Tigo ambao hufanya kazi katika vituo mbalimbali vya huduma kama vile kuongea na mtoa huduma, maduka ya Tigo pamoja na wale wanaohudumu kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumza leo hii katika kituo cha kuongea na watoa huduma wa Tigo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo Tanzania, Mwangaza Matotola, amesema maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika kwa kuonyesha ubora wa watoa huduma wa kampuni hiyo kwa wateja.
“Mwaka huu umekuwa mwaka uliojaa changamoto nyingi kwa wafanyakazi wetu wa kitengo cha huduma kwa wateja, wamejitahidi kuwa pamoja kuhakikisha maswali kutoka kwa wateja wetu yanapatiwa majibu haraka iwezekanavyo japo tusingeweza kuhudumia wateja wote kwa wakati mmoja katika maduka yetu. Pia tuliwaomba wateja wetu kuendana na mazingira yaliyokuwepo kwa kujikita zaidi katika matumizi ya huduma za kimtandao, hivyo pongezi nyingi ziende kwa timu yetu ya huduma kwa wateja kwa kutoa huduma kwa wateja wetu zenye ubora mkubwa”, amesema Matotola.
Wiki ya huduma kwa wateja ya Tigo Tanzania itaambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo kuchati moja kwa moja na wateja, kukutana na wateja pamoja na wadau wengine ili mbali na mambo mengine, kujadili namna bora ya kuboresha huduma zinazotolewa na kampuni.
“Kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu, hapa Tigo tunathamini sana mchango wa watoa huduma wetu na jinsi ambavyo wameweza kuendana na kasi ya mabadiliko, na kutokana na juhudi hizo tunaendelea kusisitiza kuwa kampuni itandelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu kila siku kama ambavyo wafanyakazi wetu wa kitengo cha huduma kwa wateja walivyoweza kuonyesha umahiri wao katika mikoa yote nchini”, amesema Matotola.
Kila wanapopata changamoto yoyote ya kimawasiliano, wateja wa Tigo wanashauriwa kutembelea maduka ya kampuni yaliyoko nchi nzima lakini pia kupata huduma kupitia njia nyingine za mawasiliano kama vile kuongea na mtoa huduma au kuchati kupitia WhatsApp, Instagram, Twitter na Facebook. Wateja watahudumiwa na watoa huduma ambao wamefuzu vyema katika kitengo hicho.
Wiki ya huduma kwa wateja itahitimishwa kwa kufanyika hafla ya utolewaji wa tuzo maalum kwa wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja. Tuzo hizo zitatolewa ili  kuwapongeza na kuwapa moyo wafanyakazi hao kwa kuendelea kutoa huduma bila kuchoka huku wakizingatia maadili ya kazi pamoja na ubora.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post