TIGO YAZINDUA KAMPENI YA ‘JAZA TUKUJAZE TENA’ ....WATEJA WANAONUNUA KIFURUSHI KUJISHINDIA DAKIKA ZA BURE, MBS,SMS NA SIMU JANJA

 Kaimu Afisa Mkuu Kitengo cha Biashara wa Tigo Tanzania, David Umoh, akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kampeni ya ‘#JazaTukuJazeTena ili kuwazawadia wateja wake. Kila mteja atakuwa mshindi kila anunuapo bando na zaidi ya simu janja 1,200 kushindaniwa.Pembeni anayeshuhudia ni Balozi wa Tigo Lucas Mhuvile "Joti" Mkutano huo umefanyika mapema leo Katika makao makuu ya Tigo.

 Balozi wa Tigo Lucas Mhuvile "Joti" akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani )  wakati wa kampeni ya ‘#JazaTukuJazeTena ili kuwazawadia wateja wake. Kila mteja atakuwa mshindi kila anunuapo bando na zaidi ya simu janja 1,200 kushindaniwa.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko William Mpinga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari 

Mkuu wa Kitengo cha Masoko William Mpinga .akiongea na waandishi wa habari mara baada ya akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kampeni ya ‘#JazaTukuJazeTena ili kuwazawadia wateja wake. Kila mteja atakuwa mshindi kila anunuapo bando na zaidi ya simu janja 1,200 kushindaniwa.Pembeni anayeshuhudia ni Balozi wa Tigo Joti Mkutano huo umefanyika mapema leo Katika ofisi za makao makuu Tigo.

Mteja atashinda dakika za bure,MBs,SMS na kupata nafasi ya kushinda simu janja zaidi ya 1,200


Dar es Salaam,Jumatatu, 25 Octoba 2020 – Kampuni ya mawasiliano inayoongoza kwa kutoa huduma za kidigitali nchini Tanzania, Tigo, leo imezindua kampeni ya siku tisini itakayofanyika nchi nzima ambayo imelenga kuwafanya wateja wote wa Tigo kuwa washindi wa zawadi mbalimbali kila wanaponunua bando za siku, wiki au mwezi.

Kampeni hii iliyopewa jina la ‘Jaza Tukujaze Tena’ inalenga kuwazadia wateja kutokana na uaminifu wao kwa kampuni ya Tigo, hivyo ndani ya kipindi cha kampeni, wateja wataweza kuzawadiwa dakika za muda wa maongezi, SMS, pamoja na MBs/GBs kila watakoponunua bando.


Pia, mbali na wateja kuzawadiwa muda wa maongezi pamoja na MBs za bure, kutakuwa na simu janja zaidi ya 1,200 ambazo pia watazawadiwa wateja. Simu janja zitakazoshindaniwa ni pamoja na Samsung Note 20, ITEL T20 pamoja na Smart Kitochi. Simu janja hizi zitashindaniwa na wateja wote wa Tigo, mawakala, viongozi wa timu za mauzo na wahudumu wakubwa wa Tigo Pesa.



Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo,Kaimu Afisa Mkuu Kitengo cha Biashara wa Tigo Tanzania, David Umoh, amesema, “Siku zote tumekuwa tukitafuta njia mpya za kuwazawadia wateja wetu pamoja na wabia wetu, na tunapoingia miezi miwili ya mwisho wa mwaka 2020, tunaamini kampeni hii itaweza kupamba sikukuu za mwisho wa mwaka. Lengo la kampeni hii ni kuhakikisha kila mteja wa Tigo anakuwa mshindi. Jaza Tukujaze Tena ni kampeni mahususi kwa ajili ya kutambua uaminifu wa wateja pamoja na wabia wetu kama kampuni”.


Pia amesisitiza juu ya namna Tigo ilivyojidhatiti kuhakikisha inaendelea kubuni bidhaa na huduma mpya zinazoendana na mabadiliko ya ulimwengu. “Ni muhimu sana kwetu tunapokuja na kampeni inayogusa maisha ya wateja wetu moja kwa moja kwa sababu wamekuwa wakitumia bidhaa zetu kila kukicha. Tigo imedhamiria kutengeneza msingi wa wateja waaminifu kwa kampuni, na kupitia kampeni hii tunalenga kufanikisha hilo,” amesema Umoh


“Tunaamini kwamba wateja wetu watafurahia kupata muda wa ziada wa dakika za kupiga simu, SMS pamoja na data ambazo tutakuwa tunawazadia ili kurahisisha maisha yao ya kila siku”, ameongeza Umoh.



Kwa wateja wetu kuzawadiwa ofa hizi za bure, wanapaswa kununua bando za siku, wiki au mwezi kupitia menu yetu ya *147*00#, Tigo Pesa App pamoja na tovuti ya Tigo. Wateja wote hawa wataweza kuingizwa moja kwa moja kwenye droo ambayo sasa itawezesha washindi wa simu janja kupatikana.



Wasambazaji wa huduma mbalimbali za Tigo pia wataweza kuingizwa moja kwa moja kwenye droo hii ili kuwa na nafasi ya kujishindia zawadi kemkem kila watakapouza bando za aina yoyote kupitia Tigo Rusha.



Tigo Tanzania inapenda kuwataadharisha wateja wake wote kwamba wawe makini na matapeli wanaoweza kuibuka kupitia mgongo wa kampeni hii. Wateja wanapaswa kufahamu kwamba, zawadi zote za bando zitakuwa zinatolewa papo hapo mara tu baada ya mteja kununua bando. Pia washindi wa simu janja wa kila siku pamoja na wiki watapigiwa simu na mfanyakazi wa Tigo kupitia namba maalumu ya kampuni mara tu baada ya droo hizo kufanyika. Ofa hii ni bure, washindi hawapaswi kutoa malipo ya aina yoyote ili kupata zawadi zao.

Wateja wote wa Tigo wanashiriki katika ofa hii.




Mwisho//.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post