WATOTO WAWILI MBARONI KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 6 KICHAKANI SHINYANGA MJINI


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawashilikilia watoto wawili wenye umri wa miaka 14 kila mmoja (majina yanahifadhiwa) wakazi wa mtaa wa Ndembezi Mjini Shinyanga kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 06. 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Oktoba 12,2020 majira ya saa tatu kasoro robo usiku huko katika mtaa na kata ya Ndembezi, manispaa na mkoa wa Shinyanga. 

“Mama mzazi mtoto huyo ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Ndembezi aligundua kubakwa kwa mtoto wake na watuhumiwa hao wawili baada ya kumlaghai mtoto huyo kwa kumnunulia pipi na kumpa hela kisha kumpeleka eneo la vichaka lililopo karibu na nyumbani kwa mtoto huyo”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

Amesema chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kingono na kwamba watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. 

Kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wazazi/walezi kwa pamoja kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili vitendo hivy vya ukatili dhidi ya watoto vikomeshwe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post