Meneja Mradi wa Huduma ya Msaada wa Kisheria kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) John Shija kutoka Shirika la PACESHI wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka wilayani Kahama
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wasaidizi wa Kisheria 'Paralegals' wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kukuza uelewa katika jamii kuhusu masuala ya sheria na matumizi ya sheria ili kuondokana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Hayo yamesemwa Jumamosi Oktoba 3,2020 na Meneja Mradi wa Huduma ya Msaada wa Kisheria kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) John Shija kutoka Shirika la PACESH Shinyanga mjini wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka wilayani Kahama yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),UNFPA na KOICA na kuratibiwa na PACESHI kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Shija alisema wajibu mkubwa wa wasaidizi wa kisheria ni kuhakikisha wanakuza uelewa kwa jamii kuhusu masuala ya sheria na matumizi ya sheria ili kuondokana na masuala ya kimila yanayokandamiza makundi ya wanawake na watoto.
"Wasaidizi wa Kisheria mna nafasi kubwa, nguvu kubwa katika kuibadilisha jamii .Kupitia mafunzo mliyopewa kuhusu ukatili wa kijinsia naamini nyinyi ndiyo mtakuwa chachu ya mwitikio wa kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kukuza usawa wa kijinsia ili mwisho wa siku tuwe na jamii yenye furaha,amani na utulivu",alisema Shija.
Shija alisema wajibu mkubwa wa wasaidizi wa kisheria ni kuhakikisha wanakuza uelewa kwa jamii kuhusu masuala ya sheria na matumizi ya sheria ili kuondokana na masuala ya kimila yanayokandamiza makundi ya wanawake na watoto.
"Wasaidizi wa Kisheria mna nafasi kubwa, nguvu kubwa katika kuibadilisha jamii .Kupitia mafunzo mliyopewa kuhusu ukatili wa kijinsia naamini nyinyi ndiyo mtakuwa chachu ya mwitikio wa kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kukuza usawa wa kijinsia ili mwisho wa siku tuwe na jamii yenye furaha,amani na utulivu",alisema Shija.
Naye Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Mwanasheria Neema Ahmed alisema ili kuondokana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake vinavyotokana na mirathi ni vyema Msimamizi wa mirathi anayeteuliwa na familia kusimamia mirathi anatakiwa kwenda mahakamani ili atambulike kisheria.
“Mume au mke akifariki dunia tusisitize mirathi ikafunguliwe mahakamani. Msimamizi wa mirathi aliyethibitishwa na mahakama ndiyo anaweza kushtaki au kushtakiwa.Ili kupata msimamizi wa mirathi ni lazima pafanyike kikao cha familia au ukoo kuteua msimamizi wa mirathi, Ufuatiliaji wa cheti cha kifo na kufungua mirathi ",alisema Neema.
Aidha alishauri jamii kuwa na utamaduni wa kuandika Wosia, akisisitiza kuwa wosia lazima uwe umesainiwa, uwe na tarehe na mashahidi wasiopungua wawili ili kupunguza migogoro ya mirathi.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Annamarie Mavenjina Nkelame aliwaomba wasadizi wa kisheria kuwashauri wananchi kutumia mabaraza ya usuluhishi wa ndoa ili kutatua migogoro ya ndoa ili kupunguza ukatili wa kijinsia.
Alizitaja baadhi ya sababu zinazopelekea mwanandoa kudai talaka ni pamoja na kutoka nje ya ndoa 'kuchepuka',ukatili, kutelekeza familia, kukimbia familia zaidi ya miaka 3, kufungwa kifungo zaidi ya miaka mitano na matatizo ya akili.
Alizitaja baadhi ya sababu zinazopelekea mwanandoa kudai talaka ni pamoja na kutoka nje ya ndoa 'kuchepuka',ukatili, kutelekeza familia, kukimbia familia zaidi ya miaka 3, kufungwa kifungo zaidi ya miaka mitano na matatizo ya akili.
"Naomba pia muwaelimishe wanaume waache kujihusisha kimapenzi na watoto, wasioe watoto kwani hii inachangia kukanyaga haki za watoto",aliongeza.
Kwa upande wao Wasaidizi wa kisheria walioshiri mafunzo hayo walikubaliana kushiriki kikamilifu kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia kamati za MTAKUWWA ngazi ya vijiji na kata na kutoa elimu kwa jamii kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye vijiji vya pembezoni.
Meneja Mradi wa Huduma ya Msaada wa Kisheria kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) John Shija kutoka Shirika la PACESHI la Shinyanga mjini wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka wilayani Kahama yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),UNFPA na KOICA na kuratibiwa na PACESHI kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia katika ukumbi wa Shinyanga Fairies Hotel Mjini Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja Mradi wa Huduma ya Msaada wa Kisheria kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) John Shija kutoka Shirika la PACESHI la Shinyanga mjini akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Meneja Mradi wa Huduma ya Msaada wa Kisheria kupitia Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) John Shija kutoka Shirika la PACESHI Shinyanga mjini akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka Halmashauri ya Msalala na Kahama Mji yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),UNFPA na KOICA na kuratibiwa na PACESHI kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia
Mwezeshaji katika mafunzo hayo,Mwanasheria Neema Ahmed akizungumza kwenye mafunzo ya siku tatu kwa Wasaidizi wa Kisheria kutoka wilayani Kahama 'Msalala na Kahama Mji' yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),UNFPA na KOICA na kuratibiwa na PACESHI kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia
Mwezeshaji katika mafunzo hayo,Mwanasheria Neema Ahmed akitoa mada kuhusu Mirathi
Mwezeshaji katika mafunzo hayo,Mwanasheria Neema Ahmed akifafanua umuhimu wa kuandika Wosia
Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Annamarie Mavenjina Nkelame akitoa mada ya Ndoa na Sheria zinazolinda watoto.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Annamarie Mavenjina Nkelame akiwaomba wasadizi wa kisheria kuwashauri wananchi kutumia mabaraza ya usuluhishi wa ndoa ili kutatua migogoro ya ndoa ili kupunguza ukatili wa kijinsia.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Annamarie Mavenjina Nkelame akiendelea kutoa mada ya ndoa.
Wasaidizi wa kisheria wakiwa ukumbini.
Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya Msalala, Asinath Remtula akizungumza kwenye mafunzo hayo
Msaidizi wa Kisheria Zephania Paul akizungumza katika mafunzo hayo.
Msaidizi wa Kisheria Philipo Jackson akichangia hoja ukumbini
Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali halmashauri ya wilaya ya Msalala, Giringai Osward Mahemba akizungumza katika mafunzo hayo.
Msaidizi wa Kisheria Divid Nkowa akizungumza katika mafunzo hayo.
Social Plugin