Na Marco Maduhu Shinyanga.
Shirika la Investment in Children and their Societies (ICS) limeungana na Serikali mkoani Shinyanga kuzindua mpango mkakati wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ambao utadumu kwa muda wa miaka mitano, ili kusiwepo tena na matukio hayo mkoani humo zikiwemo mimba na ndoa za utotoni.
Mpango huo umezinduliwa jana katika Kata ya Segese halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Shinyanga, likiwamo Shirika la ICS, AGAPE, Rafiki SDO, WFT,Mtandao wa Kijinsia Tanzania TGNP, UN WOMEN, UNFPA na KOICA.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amesema Serikali ya mkoa huo ni ya kwanza hapa nchini kati ya mikoa 26 , kuzindua mpango wake mkakati wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Tumezindua mpango huu mkakati wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ambao utadumu kwa muda wa miaka mitano, kuanzia (2020-2025) kwa kuonyesha dira ya mkoa, na kubainisha changamoto zilizopo katika mkoa wetu ambazo ni chanzo cha matukio haya na kuzifanyia kazi,”amesema Telack.
“Mashirika yote yasiyo ya kiserikali katika utekelezaji wao wa miradi ya mpango mkakati wa kitaifa wa Serikali wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA, watautumia mpango huu ambao tumeuzindua leo na kuwa kama dira yao,”ameongeza.
Aidha amesema kazi ya kuandaa mpango huo umefanywa na viongozi wa Serikali mkoani Shinyanga, kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo mkoani humo, likiwamo Shirika la ICS, Women Fund Tanzania (WFT) ,Rafiki SDO, pamoja na AGAPE, ambapo pia wameshiriki kufadhili uzalishaji wa nyaraka za vitabu na uzinduzi wa kitabu hicho cha mpango mkakati.
Ameitaka jamii ya mkoa wa Shinyanga, kuachana na matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, pamoja na kuacha kuendekeza mila potofu ambazo ni kandamizi zilizopitwa na wakati.
Amesema dhamira ya mkoa huo ni kuona kunakuwepo na usawa wa kijinsia kwenye nyanja zote, zikiwemo shughuli za kiuchumi, pamoja na watoto wa kike kuwa sawa kimasomo na wa kiume, na kuacha tabia ya kuwaozesha ndoa za utotoni na kuzima ndoto zao.
Naye Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sifuni Msangi, ameipongeza Serikali ya mkoa wa Shinyanga, kwa kuzindua mpango wake mkakati wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ambao ni moja ya utekelezaji wa MTAKUWWA, ambao umelenga ifikapo mwaka 2025 matukio hayo ya ukatili yawe yamepungua.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Investment in Children and their Societies (ICS) Kudely Sokoine, ambao ni miongoni mwa wadau wakubwa walioshiriki kuandaa mpango mkakati wa mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, amesema wao wataendelea kuutumia mpango huo katika kutekeleza miradi yao ambayo tayari shughuli hizo wanazifanya ndani ya jamii.
Amesema ili kuwa na Taifa zuri, lazima kuwepo na usawa wa kijinsia, na ndio maana Shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na Serikali pamoja na mashirika mengine, kupambana kutokomeza matukio hayo ya ukatili ndani ya jamii dhidi ya wanawake na watoto.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (katikati) akizundua kitabu cha mpango mkakati wa Serikali mkoani humo wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kushoto kwake ni Mkurugenzi mkazi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa na Idadi ya watu (UNFPA) Dk. Willfred Ochani, na kulia kwake ni Mkurugenzi mkazi kutoka Shirika la maendeleo la Korea KOICA Kyucheol Eo, na wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine.
Uzinduzi wa kitabu cha mpango mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ukifaana, na wadau kushangilia kwa kupiga makofi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akizungumza kwenye uzinduzi wa kitabu cha mpango mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sifuni Msangi, akiipongeza Serikali ya mkoa wa Shinyanga, kwa kuzindua mpango wake mkakati wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango mkakati wa Serikali mkoani humo wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mkurugenzi wa Shirika la Investment in Children and their Societies (ICS) Kudely Sokoine, akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango mkakati wa Serikali wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akimkabidhi kitabu cha mpango huo mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Mkurugenzi mkazi kutoka shirika la umoja wa mataifa na idadi ya watu (UNFPA) Dr. Willfred Ochani.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akimkabidhi kitabu cha mpango huo mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Mkurugenzi mkazi kutoka Shirika la maendeleo la korea Koica Kyucheol Eo.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akimkabidhi kitabu cha mpango huo mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Makamu mwakilishi wa mashirika yanayojihusisha na usawa wa kijinsia (UN WOMEN) Julia Broussard.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akimkabidhi kitabu cha mpango huo mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Mwakilishi kutoka ofisi ya Rais.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akimkabidhi kitabu cha mpango huo mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akimkabidhi kitabu cha mpango huo mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akimkabidhi kitabu cha mpango huo mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Taraba.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akimkabidhi kitabu cha mpango huo mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Debora Magiligimba.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akimkabidhi cheti afisa miradi kutoka Shirika la ICS Sabrina Majikata kwa niaba ya Shirika la Women Fund Tanzania (WFT).
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akimkabidhi cheti afisa miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani.
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitabu cha mpango mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitabu cha mpango mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Wananchi, pamoja na watoto, wakiwa kwenye uzinduzi wa kitabu cha mpango mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitabu cha mpango mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Wadau wa maendeleo wakiwa kwenye uzinduzi wa kitabu cha mpango mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Uzinduzi wa kitabu cha mpango mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ukiendelea.
Uzinduzi wa kitabu cha mpango mkakati wa Serikali mkoani Shinyanga wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ukiendelea.
Awali mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akiingia uwanjani tayari kwa kuzindua kitabu cha mpango huo mkakati, akiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, pamoja na mkuu wa wilaya ya Kshapu Nyabaganga Taraba.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Social Plugin