POLISI DAR WAONYA..."OLE WAO WANAOPANGA KUINGIA BARABARANI KUANDAMANA, KITAKACHOPAWATA WATAJUTA"

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa onyo kali kwa mtu, watu au kikundi chochote cha watu ambao wanapanga kuingia barabarani kuandamana kwani halitawaachia na kitakachowatokea wasijutie.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari jana jioni Oktoba 30,2020 kwamba wanazo taarifa kuna watu wamekaa vikao vya siri wakipanga mipango ya kuingia barabarani kuandamana.

Amefafanua uchaguzi ulikuwa umamalizila salama na amani lakini baada ya matokeo kuanza kutangazwa vimeibuka  vikundi vya watu wengine wakiwamo waliogombea  nafasi mbalimbali ambao wanaendelea kufanya vikao ya siri lakini mipango yao ni kutaka kwanza kuingilia mchakato wa  kutangaza matokeo hayo yanayoendelea.

Pia wanajaribu kuhamasisha wafuasi wao kuingia mtaani , na jambo linaloshangaza kufanya hivyo wengine wanaopanga mipango hiyo wameshindwa Hai, wameshindwa Kilimanjaro, wameshindwa Arusha lakini wamejikusanya  jijini Dar es Salaam kama eneo ambalo ni shamba la bibi, wanataka kufanya vurugu.

"Nimekuja kwa umma kutoa onyo kwao , kipindi cha kampeni ambacho tulikuwa wastaarabu sana ,tumewapa nafasi ya kunadi sera zao, na kipindi hiko kimeshikwa ,sasa tuko katika kutekeleza dhima na dhumuni la Jeshi la Polisi ambalo ni kulinda maisha ya watu na mali lakini ni pamoja na kuwalinda viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ambao wanaendelea kukamilisha matokeo kwenye majimbo ambayo nafas ya urais yanaendelea kutolewa.

"Nitoe onyo wananchi mnaokaa Dar es Salaam wapuuzeni ,anayetaka kuingia mtaani aingie yeye, kama ana mke atangulize mke wake, kama ni mme atangulie yeye , tukutane naye tumejipanga na hatuna mjadala katika hili, tunachotaka kuhakikishia watanzania wote wanaokaa Dar es Salaam , mko salama na jeshi limesimama na linaendelea kufanya kazi yake, tumezunguka maeneo yote, tumekaa kuhakikisha mtu atakayeachiwa afanye lile analolifikiria.

"Niwaombe wale ambao watapata taarifa watu kutaka kuingia barabarani watupe taarifa mapema, tunaendelea kufuatilia lakini mahali popote watakapoanzia tutawa labda umbali wa hatua 10 na wasijutie kitakachowapata , kwasababu tumeamua kuhakikisha hatuwapi nafasi kuchezea demokrasia hii ambayo kimsingi kinachotangazwa ni maamuzi ya wananchi wenyewe,"amesema.

Amesisitiza hakuna sababu ya kwenda kugombea kama hauko tayari kushinda au kushindwa, yoyote anayeingia kwenye ushindani ategemee mawili, kupewa ama kukosa,waliokosa basi wavumilie na wanakatibishwa mwaka 2025 lakini kwa sasa mchezo wa kampeni kushawishi,kuvuruga havina nafasi."Hayo ndio maamuzi ya Watanzania ,yanayoendelea kutangazwa ni lazima tuyaheshimu na yoyote atakayepuuza asilie na kile atakachokutana nacho.Tumesimama kuhakikisha hatumuachii mtu nafasi ya kufanya lolote, na narudia tena mtu asijutie kwa lile atakalokutana nalo.

" Niwaombe watanzania wote wapuuze vitendo vya kuingia barabarani havina afya,havina baraka, lakini pia vinakinzana na demokrasia  yenyewe ,wananchi wameamua halafu unataka wagomee,unagomea ili umuongoze nani".

CHANZO- MICHUZI BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post