WANAWAKE KANISA LA PHILADELPHIA MIRACLE TEMPLE NDEMBEZI SHNYANGA WAFANYA SHEREHE

 

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Philadelphia Miracle Temple la Ndembezi mjini Shinyanga pamoja na Mama Mchungaji, Evarine Msangi wakipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa waumini wa kanisa hilo wakati wa kilele cha sherehe ya akina mama kanisani hapo Jana Jumapili

Na Shinyanga Press Club Blog
Waumini wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample lililoko Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kutulia mbele za Mungu na kulitafakari neno lake, ikiwa ni pamoja na kufunga na kuomba ili waweze kuzidishiwa yote wanayohitaji kwa Muumba wao.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti Msaidizi wa Chama cha Wanawake wa kanisa hilo, Elizabeth Anania alipokuwa akihubiri neno la Mungu katika ibada ya Jumapili ambayo ilikuwa siku ya kilele kuhitimisha sherehe ya wanawake kanisani hapo.

Elizabeth amesema kuwa waumini wengi wamekuwa hawatulii kwa bwana wamekuwa wakitangatanga,huku na wakikimbilia miujia bila kutambua kuwa miujiza inapatikana pale mtu anapotulia kwa mungu na kumuomba ili aweze kujibiwa mahitaji yake.

Aliongeza kwa kueleza kuwa mtu anapotulia katika Bwana anapokea hata asiyoyaomba, anapata furaha na amani na kuzidishiwa yote anayoyahitaji.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wanawake wa Kanisa la Philadelphia Miracle Temple, Suzy Butondo ambaye pia ni Mzee wa kanisa, katika mahubiri aliwaomba wanawake wote na waumini wa kanisa hilo waombe katika roho na kweli, waombe katika utakatifu na waombe katika mapenzi ya mungu ili waweze kujibiwa mahitaji yao.

Suzy amesema ili muombaji aweze kujibiwa anatakiwa ajitakase akae katika uwepo wa mungu ili amwambie mungu mahitaji yake, kwa sababu mungu hujibu maombi ya waumini wanaoomba katika roho na kweli.

"Ukiomba katika roho na kweli mkono wa bwana utashuka na kukuondoa ulipo na kukuweka kwenye sehemu nzuri na kuzuia nguvu za shetani zinazokuja kwako kwa ajili ya kukudhuru," amesema Suzy.

Pia amesema waumini wote wanatakiwa kuwa na neno la mungu ndani ya mioyo yao ili wasije kutenda dhambi, kwa sababu mtu akiwa muombaji na akiwa na neno la mungu lazima atakuwa na hofu ya mungu hatathubutu kutenda dhambi, neno la mungu kutoka Zaburi 119:11 linasema.

Aidha amesema muombaji mzuri anaeomba katika roho na kweli lazima anakuwa na furaha na amani kila wakati kwa sababu mungu anakaa pamoja nae, hivyo ni vizuri wanawake na watu wote wakajikita kwenye maombi ili waweze kuwa na furaha na amani siku zote za maisha yao.

"Tusikate tamaa katika maisha tunachotakiwa ni kudumu katika maombi kwani hakuna kinachoshindikana mbele za Mungu, Mungu wetu hachelewi wala hawahi anajibu kwa wakati wake wewe omba katika roho na kweli jitakase ipo siku utajibiwa na utaushuhudia ukuu wa mungu," amesema Suzy.

Naye Mwenyekiti wa Wanawake wa Kanisa hilo, Dionisio Herman amesema wanawake ni jeshi kubwa na ni waombolezaji, hivyo ni vizuri wakatulia mbele za bwana na wakamuomba Mungu katika roho na kweli ili aweze kuwajibu mahitaji mbalimbali wanayomuomba.
Mchungaji Laizer Baraka na mkewe Evarine Msangi wakiwa kanisani hapo wakati wa sherehe hiyo
Mama Mchungaji, Evarine Msangi (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa muumini wa kanisa hilo
 
Waumini wakipeleka zawadi katika sherehe yao kanisani hapo

Mama Mchungaji, Evarine Msangi akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa waumini wanawake wakati wa sherehe yao
Akina mama waumini wa kanisa hilo wakipeleka zawadi

Waumini wakifurahia katika sherehe hiyo
Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wa Kanisa hilo, Dionisio Herman (kushoto) akiwasilisha zawadi ya akina mama
Mchungaji Msaidizi, Anania Clement na Mkewe, Elizabeth Anania wakiwa kanisani hapo wakati wa sherehe hiyo
Mchungaji Msaidizi, Charles Kwilemba akipokea zawadi ya akina mama kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wa Kanisa hilo,Dionisio Herman (kushoto)
Waumini wakisoma risala kanisani hapo

 Wanawake wakiimba kwaya katika kusherehekea sikukuu yao

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post