WADAU WATAKA MTOTO WA KIKE KULINDWA DHIDI YA CHANGAMOTO


Baadhi ya Wanafunzi wa shule anuai za sekondari Kahama wakiserebuka kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni, lililoandaliwa na taasisi ya C- Sema na kushirikisha wadau mbalimbali wanaotetea haki za watoto wa ujumla.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Msalala, Bi. Neema Katengesya kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni.
Miss Tanzania mwaka 2005, Nancy Sumari na mgeni rasmi kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni akisalimiana na maofisa wa TEN/MET pamoja na wanachama wanaounda mtandao huo. 
Miss Tanzania mwaka 2005, Nancy Sumari na mgeni rasmi kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni akisalimiana na wanachama wanaounda mtandao wa TEN/MET. 
Miss Tanzania mwaka 2005, Nancy Sumari ambaye ni mgeni rasmi akisaini kitabu cha wageni ndani ya Banda la Tenmet kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni.
Miss Tanzania mwaka 2005, Nancy Sumari ambaye ni mgeni rasmi akipokea vipeperushi ndani ya Banda la Tenmet kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule za sekondari Kahama walioshiriki Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni, wakipata elimu kwenye banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).
Wanafunzi wa shule za sekondari Kahama walioshiriki Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni, wakipata elimu na vipeperushi vyenye jumbe mbalimbali kwenye banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).
Ofisa TEHAMA toka Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Kenneth Nchimbi (kulia) akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea kwenye banda lao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Msalala DC, Dk. Ntauwa Kilagwile kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni.
Mwenyekiti wa C-Sema, Balozi Bi. Nyasigara Kadege kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni.
Miss Tanzania mwaka 2005, Nancy Sumari ambaye ni mgeni rasmi akizungumza na wanafunzi kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni.
Miss Tanzania mwaka 2005, Nancy Sumari ambaye ni mgeni rasmi akimkabidhi zawadi ya baskeli mmoja wa wanafunzi aliyeibuka mshindi wa kwanza wa mbio za baskeli kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni.

Wanafunzi wakijiandaa kushindana mbio za baskeli kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni.
Wadau mbalimbali kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule za sekondari Kahama walioshiriki Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni, wakipata elimu kwenye banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET).
Baadhi ya Wanafunzi wa shule anuai za sekondari Kahama wakiserebuka kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni, lililoandaliwa na taasisi ya C- Sema na kushirikisha wadau mbalimbali wanaotetea haki za watoto kwa ujumla.

**

Na Mwandishi Wetu, Kahama

TAASISI mbalimbali zimepaza sauti zikiwataka wazazi na jamii kwa ujumla kumlinda mtoto wa kike dhidi ya changamoto anuai zinazowakabili zikiwemo mila potofu ambazo bado ni kikwazo cha katika kutimiza ndoto ya mtoto huyo.

Kauli hizo zimetolewa hivi karibuni Mjini Kahama kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Ulimwenguni, lililoandaliwa na C- Sema na kushirikisha wadau mbalimbali wanaotetea haki anuai za watoto kiujumla.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mwenyekiti wa C-Sema, Balozi Bi. Nyasigara Kadege aliwataka kuhimiza elimu kwa watoto wa kike na kupewa fursa ya kusikilizwa ili waweze kutimiza ndoto zao. 

"...Mimi baba yangu na mama yangu wasingenipeleka shule leo nisingekuwa na nafsi hii, nawaombeni wazazi na walezi tuwape fursa ya kuwasikiliza watoto wa kike kuanzia ngazi ya familia hadi jamii," alisema Balozi Bi. Nyasigara Kadege.

Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Msalala, Bi. Neema Katengesya aliwataka wazazi jamii ya kisukuma wanaobaagua elimu kwa mtoto kwa kike kuachana na mila hizo na kutoa fursa ya elimu ili jamii hiyo ya kike iweze kuibadili jamii nzima kwa elimu waliopatiwa na wazazi wao. Aliwataka pia jamii hiyo ya wasukuma kuacha mila za kumtakasa mtoto wa kike (kuoga nsamba) kana kwamba anamkosi jambo ambalo ni udhalilishaji. 

"...Hakuna mtoto wa kike anayezaliwa na mkosi, fikra hizi ni potofu tuziache mara moja, naomba tuache kuwaogesha watoto madawa eti tunawatoa mkosi, jambo la msingi ni kuwalea watoto wetu kimaadili na kuwatunza vizuri. Mtoto akiwa na tabia njema na maadili mema hawezi kuwa na mkosi, utakuwa na mkosi kama unatabia mbaya ya kujipitisha na kujionesha vibaya kwenye jamii," alisema Bi. Katengesya.

Akiwasilisha Ujumbe wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kwa wanafunzi wa kike waliotembelea banda la Tenmet kwenye kongamano hilo, Ofisa TEHAMA, Bw. Kenneth Nchimbi alisema Siku ya Kimataifa ya Binti 2020 ni ya kipekee. Aidha alisena Tenmet inatambua kuwa mwaka huu (2020) kauli mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Binti ni "Sauti yangu, Usawa Wetu". Kauli hii inaangalia kwa umakini namna wasichana duniani wanaongoza njia.

"...Kila siku wasichana wanakabiliwa na vikwazo mbalimbali kama vile umasikini, mila na desturi potofu, miundo mbinu mibovu, ukatili na unyonge na hivyo kukosa elimu. Katika kuadhimisha siku hii, TEN/MET inaendelea kukazia uharaka wa kuondolewa vikwazo vyote vinavyopunguza nafasi ya msichana kuwa mwongoza njia." 

Alisema afisa huyo wa TEHAMA toka Tenmet akizungumza na baadhi ya mabinti waliotembelea banda lao katika kongamano hilo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Msalala DC, Dk. Ntauwa Kilagwile aliitaka jamii kuungana na Serikali kuwapatia fursa ya elimu watoto wote bila ubaguzi, kwani ndio lengo la kutoa elimu bila ada kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne kwa sasa. Tuiunge mkono Serikali kwa kuhakikisha tunapeleka watoto wetu shule bila kuwabagua," alisema Dk. Ntauwa Kilagwile akihutubia kongamano hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post