Angalia Picha : MAHAFALI YA SHULE YA AWALI NA DARASA LA SABA 2020 SHULE YA MSINGI LITTLE TREASURES

Na Marco Maduhu  -Shinyanga. 

Shule ya msingi Little Treasures iliyopo manispaa ya Shinyanga, imefanya mahafali ya nne kuwaaga wanafunzi wake waliohitimu elimu ya msingi darasa la saba 2020, pamoja na wanafunzi wa awali ambao wataingia darasa la kwanza mwaka 2021.


Mahafali hayo yamefanyika leo shuleni na kuhudhuriwa na wazazi, huku mgeni Rasmi akiwa ni Mgombea ubunge wa viti maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga kupita Chama Cha Mapinduzi (CCM(. 

Akizungumza kwenye mahafali hayo, Mayenga, amewaasa wazazi na walezi wakawalee vyema wanafunzi hao ambao wamehitimu elimu ya msingi, ili waendelee kuwa na maadili mema kama walivyofundishwa shuleni hapo, na siku matokeo yakitoka wakutwe wakiwa salama na kisha kuendelea na kidato cha kwanza. 

Amesema wanafunzi hao wanapswa kulindwa kwa kiwango cha hali ya juu kwa sababu wameshatoka mikononi mwa walimu ambao walikuwa wakiwalea vizuri, na kwa maadili mema, na sasa wanarudi mikononi mwa wazazi, na kuwataka wapunguze ubize wa maisha na kuwalea watoto. 

“Natoa ushauri kwa wazazi tupunguze u -busy wa maisha na tuwalee watoto wetu vizuri kwa maadili mema, na pia tuache kupigana mbele ya watoto, tuta waaribu kisaokolojia na hatimaye kushusha uwezo wao wa kimasomo,” amesema Mayenga. 

“Natoa pia wito kwa wanafunzi ambao mmehitimu leo elimu ya msingi, mkajitunze majumbani na kuacha kudhulula hovyo, na kutojiingia kwenye makundi mabaya ambayo yatawasababishia kuzima ndoto zenu,”ameongeza. 

Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya msingi Little Treasures Paulo Kiondo, akisoma risala ya Shule hiyo, amesema wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi ni 91, huku wanafunzi wa awali wakiwa 95, ambapo jumla ya wanafunzi wote ni 843. 

Amesema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma kwenye mitihani ya kitaifa, ambapo kwa matokeo ya mwaka 2019 ya darasa la saba ilishika nafasi ya 4, pamoja na kuingiza wanafunzi watatu (3) kwenye 10 bora kitaifa, mvulana mmoja na wasichana wawili. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo Lucy Msele, aliwapongeza wazazi kwa kuendelea kuwa na ushirikiano na walimu, ambapo ndiyo moja ya siri ya mafanikio shule hiyo kufanya vizuri kitaaluma, huku akiahidi kuendelea kuufanyia kazi ushauri wao, ambapo pia wameshaanzisha na Sekondari, na sasa ina wanafunzi wa kidato cha Tatu. 

Pia alimpongeza Rais John Magufuli kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwenye mapambano ya maambukizi ya virusi vya Corona, na hatimaye kuisha hapa nchini, ambapo wanafunzi waliendelea na masomo yao vizuri, na kuahidi watafulu wote kwenda kidato cha kwanza. 

Aidha Rose Ngatale akisoma risala kwa niaba ya wazazi wanaosomesha watoto shuleni hapo, alipongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuwalea watoto wao kimaadili pamoja na kuwapatia taaluma, na kuahidi kwenda kuyaendeleza yale ambayo wamefundishwa shuleni hapo. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mgeni Rasmi Lucy Mayenga akizungumza kwenye mahafali ya Little Treasures.
Mkurugenzi wa Shule Little Treasure Lucy Msele, akizungumza kwenye mahafali.
Meneja wa Shule ya Little Treasures Mwita Peter, akizungumza kwenye mahafari hayo na kubainisha moja ya changamoto ambayo inawakabili shuleni hapo ni ukosefu wa umeme, ambapo kwa sasa wanatumia Sola.
Mhitimu Marry Paul akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliohitimu darasa la saba.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paulo Kiondo, akisoma risala ya shule hiyo.
Mwakilishi wa wazazi Rose Ngatale akisoma risala kwa niaba ya wazazi wanaosomesha watoto shuleni hapo
Wahitimu wa darasa la saba wakiwa kweye mahafali yao.
Wahitimu wa darasa la saba wakiwa kweye mahafali yao.
Wahitimu wa masomo ya awali wakiwa kwenye mahafali yao.
Wahitimu wa masomo ya awali wakiwa kwenye mahafali yao.
Wahitimu wa masomo ya awali wakiwa kwenye mahafali yao.
Wanafunzi wanaobaki wakiwa kwenye mahafali ya wahitimu wa darasa la saba.
Wanafunzi wa Sekondari ya Little Treasure wakiwa kwenye mahafali ya wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo.
Wanafunzi wa Sekondari ya Little Treasure wakiwa kwenye mahafali ya wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali.
Mgeni Rasmi Lucy Mayenga akikata keki ya wahitimu wa darasa la saba.
Mgeni Rasmi Lucy Mayenga akikata keki ya wahitimu wa darasa la awali.
Mgeni Rasmi Lucy Mayenga akiwalisha keki wahitimu wa darasa la awali.
Mgeni Rasmi Lucy Mayenga akiwalisha keki wahitimu wa darasa la saba.
Mgeni Rasmi Lucy Mayenga akigawa vyeti wa wahitimu wa darasa la saba.
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea.
Mgeni Rasmi akigawa vyeti kwa wahitimu wa darasa la awali.
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea.
Wanafunzi wanaobaki shuleni hapo, wakitoa burudani nyimbo ya mwanamziki Diamond Platnum, "Kalantini"
Burudani zikiendelea kutolewa.
Burudani zikiendelea kutolewa.
Wafanyakazi wa shule ya Little Treasures wakiongozwa na mkurugenzi pamoja na meneja wa shule hiyo wakitoa burudani.
Wahitimu wakitoa darasa la saba wakitoa burudani.
Wahitimu darasa la awali wakitoa burudani.
Wazazi wakitoa zawadi kwa Mkurugenzi wa Shule ya Little Treasures Lucy Msele, pamoja na meneja wa shule hiyo Mwita Peter.
Wazazi wakitoa zawadi kwa Mkurugenzi wa Shule ya Little Treasures Lucy Msele
Awali wahitimu wa darasa la saba wakiwa kwenye maandamano.
Awali wahitimu wa darasa la saba wakiwa kwenye maandamano.
Awali wahitimu wa darasa la awali wakiwa kwenye maandamano.
Awali wahitimu wa darasa la awali wakiwa kwenye maandamano.
Awali wahitimu wa darasa la saba wakiingia ukumbini kwa ajili ya kuendelea na mahafari yao.
Awali wahitimu wa darasa la awali wakiingia ukumbini kwa ajili ya kuendelea na mahafari yao huku wakipokewa na mkurugenzi wa shule hiyo ya Little Treasure Lucy Msele.

Na Marco Maduhu-Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post