Mgombea wa Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe, ametoa sababu ya kuandika barua iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikieleza kuhusu kujitoa kwenye kinyanganyiro cha Urais wa Tanzania bara.
Membe kupitia ukurasa wake wa Twitter leo, amethibitisha kuwa barua hiyo iliyosambaa mitandaoni kuwa ni ya kweli na yeye ndiye aliyeandika barua hiyo.
“Barua inayosambaa ya tarehe 24/9 ya kujiondoa kwenye mbio za Urais ni ya kweli, niliandika baada ya kutofautiana na msimamo wa Viongozi wangu wa kutaka nimuunge mkono Tundu Lissu. Hata hivyo barua hiyo ilikataliwa kwa sababu maneno " msimamo wa viongozi wangu" yanawatia hatiani.” amesema Bernard Membe
Aidha katika barua hiyo inayosambaa iliyoelekezwa kwa mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif, na Katibu Mkuu wa cha hicho , Membe aliahidi kujikita katika kuwasaidia madiwani na wabunge wote wa chama hicho.
Social Plugin