WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam huku wakiwa wameshikilia madafu mikononi
WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam huku wakinywa maji ya dafu kama wanavyoonekana
WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam wakiwa wamekaa kwenye jamvi na wengine wamesimama
WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam
WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakikata keki ikiwa ni ishara ya wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
BENKI ya I&M
Tanzania imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kwa kutambua mchango
muhimu unaotolewa na fanyakazi wake katika kuwahudumia wateja wao kwa
viwango vya juu na kuhakikisha kuwa wanakuwa wenye furaha wakati wote.
Hafla
hiyo ilifanyika maktaba square jijini Dar es Salaam katika makao makuu
ya benki hiyo, ikiambatana na shughuli mbalimbali kwa wateja kama
ishara ya shukrani kwa wateja wanaothaminiwa na pia wafanyakazi wake
ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu muhimu la kutoa huduma bora kwa
wateja wakati wote.
Miongoni mwa shughuli za
kusherehesha hafla hiyo na wiki ya huduma kwa wateja zilizofanywa na
benki hiyo ni pamoja na Maofisa wa juu na waandamizi wa benki hiyo
akiwamo Afisa Mtendaji Mkuu, walichukua jukumu la kuhudumia wateja
katika matawi mbalimbali kwa siku ya jana.
Sheherehe
hiyo ya wiki nzima ni matokeo ya kujitolea kwa benki hiyo ya I&M
katika kuongeza ushiriki wa wafanyakazi katika kuunga mkono kaulimbiu ya
mwaka huu ya siku hiyo inayosema kuwa, ‘Timu ya ndoto’.
Mbali
na ushiriki wa watendaji wakuu, maafisa waandamizi katika kufanya
jukumu la huduma kwa wateja, pia wafanyakazi wote wa benki hiyo
walipokea barua binafsi za shukurani kwa bidii yao na kujitolea kwao
katika kuleta matokeo chanya na furaha kwa wateja katika benki hiyo.
Mkuu
wa Mauzo ya rejareja wa benki hiyo, Lilian Mtali alisema katika
kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wanataka onyesha thamani ya watoa
huduma kwa wateja.
“Sisi benki ya I&M tunataka
kutumia wiki hii ya huduma kwa wateja kuhakikisha kuwa tunawaonyesha
thamani na ukarimu wateja wetu,lakini pia kuunga mkono na kutambua kazi
nzuri na kubwa inayofanywa na maafisa wa huduma kwa wateja kama dawati
namba moja ambalo ni nembo na kilelezo cha huduma bora za benki.
“Kwani
sote tunatambua kuwa dawati la huduma kwa wateja ndilo limebeba sura na
kilelezo cha huduma bora zinazotolewa na benki, wamekuwa wakaifanyakazi
kwa bidi kwani hata pale wateja wanapokuwa na jazba, wao wamekuwa
wakijitahidi kuhakikisha kuwa wanakamilisha mahitaji yao na kuwaacha
wakiwa na furaha jambo ambalo ni kipaumbele cha benki,” alisema Lilian.
Wiki
ya Huduma kwa Wateja ni maadhimisho ya umuhimu wa huduma kwa wateja na
ya watu ambao wanahudumia na kusaidia wateja kila siku.
Hafla
hiyo huadhimishwa kila mwaka wakati wa wiki ya kwanza ya Oktoba na
wafanyabiashara wote na mashirika yanayolenga huduma kote ulimwenguni,
ambayo hutambua umuhimu wa kutoa huduma bora kwa wateja.
Social Plugin