CHANGAMOTO za wizi wa fedha ,utapeli
na dhuluma zilizokuwa zikiwakabili wakulima wa mazao ya kimkakati huenda sasa
zitafika kikomo baada ya Benki ya CRDB kupata ufumbuzi wa changamoto hizo kwa
kuanzisha akaunti maalumu ya Fahari Kilimi maalumu kwa wakulima.
Wakati dunia ikiwa katika wiki ya
huduma kwa wateja iliyobeba kauli mbiu ya “Dream Team” Mashirika ya umma ,ya
binafsi pamoja na taasisi mbalimbali za fedha nchini zimeungana katika
maadhimisho ya wiki hii huku CRDB wakiweka wazi namna ambavyo wamejipanga
kumsaidia mkulima.
Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya
Kaskazini Chiku Issa amesema wakulima katika maeneo mbalimbali wamekuwa
wakipokea fedha zao kwa njia ya pesa taslimu .
“Hili limetokea zaidi maeneo ambayo
yana mazao ya kimkakati kama Pamba ,Kahawa,Tumbaku,Chai na Katani ,wengi wa
wakulima hawa walikuwa wanapokea kwa njia ya Cash”alisema Chiku .
“Kulikuwa na ubadhilifu mkubwa watu
walikuwa hawapewi fedha zao sahihi laikini pia ilikua ni hatari sana wengi wao
walikuwa wanapoteza fedha kwa matapeli lakini pia kwa kuibiwa” aliongeza Chiku.
Amesema CRDB imekuja na bidhaa nyingi
tofauti ambazo zinagusa jamii kwa kila kada ambapo akaunti ya kilimo
ni maalumu kwa wakulima na kwamba haina makato ya aina yeyote na itasaidia
kuendeleza kilimo.
Chiku amesema CRDB itaendelea
kuboresha huduma zake ili kila mtanzania na kila mteja wa CRDB ziweze kumgusa
na kuweza kupata mikopo kwa urahisi ili kuboresha maisha yao na
kwenda na uchumi wa kati.
“Benki inaungana na taasisi
nyingine duniani kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kuwahudumia na
kuwahamasiha kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hii ili kuboresha
maisha yao.”alisema Chiku.
Wiki ya huduma kwa wateja huadhimishwa kila mwaka ifikapo mwezi Oktoba ambapo taasisi,mashirika na kampuni mbalimbali huadhimisha kwa kurejesha kwa jamii sehemu ya faida iliyopatikana.
Social Plugin