Kamati ya Maadili ya Taifa imesitisha adhabu ya kufungiwa Wagombea Ubunge wa NCCR Mageuzi, James Mbatia (Vunjo) na Anthony Komu (Moshi V) na kuwaruhusu kuendelea na kampeni.
Walifungiwa kufanya kampeni (17-23 Oct) kwa kutumia vipeperushi visivyoidhinishwa na Msimamizi wa Uchaguzi
Uamuzi huo umetolewa jana Oktoba 20,2020 baada wajumbe 13 kati ya 17 walioshiriki kikao cha kusikiliza rufaa za wagombea hao kupiga kura na kuafiki kutenguliwa kwa adhabu hizo zilizotolewa Oktoba 17, 2020.
Kikao cha kamati ya maadili jimbo la Vunjo kilimtia hatiani Mbatia kwa kutumia kipeperushi ambacho hakijaidhinishwa na msimamizi na Komu akapatikana na hatia ya kutumia bango ambalo halikuidhinishwa.
Wagombea hao wakapewa adhabu ya kutofanya kampeni kwa siku saba kuanzia Oktoba 17 hadi Oktoba 23, 2020 lakini hawakuridhika na adhabu hizo wakaamua kukata rufaa kamati ya maadili ya taifa.
Social Plugin