MWENYEKITI wa zamani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM) Abdiely Makange akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuwataka watanzania kumpigia kura za kishindo Rais Dkt John Magufuli kutokana na kasi ya maendeleo iliyopo hapa nchini
MWENYEKITI wa zamani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM)
Abdiely Makange akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuwataka
watanzania kumpigia kura za kishindo Rais Dkt John Magufuli kutokana na
kasi ya maendeleo iliyopo hapa nchini
MWENYEKITI wa zamani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM) Abdiely Makange amewataka wakazi wa mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuchagua
viongozi wa chama cha Mapinduzi(CCM) akiwemo Rais Dkt John Magufuli ili kuhakikisha mkakati wa serikali
ya chama tawala ya kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi unafanikiwa
Makange aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisemaserikali ya awamu ya tano ilifanya mabadiliko makubwa
ya kiuchumi katika mkoa huo kwa kuimarisha miundo mbinu mbalimbali
ikiwemo Bandari,Barabara,Reli na Umeme.
Alisema
takribani shilingi Bilioni 372 zilitolewa na serikali kwa ajili ya
kuongeza kina cha maji kwenye Bandari ya Tanga hatua ambayo imewezesha
Meli kubwa kutoka ndani na nje ya nchi kutia nanga kwenye Bandari hiyo.
"Tunaona
ambavyo sasa wafanyabiashara wa soko kama mgandini na mengineyo ambayo
wanauza bidhaa zao kwenda ZanzÃbar Meli ya Azam inatia nanga kwenye
bandari ya Tanga na kununua biadhaa mbalimbali kutoka Tanga",alisema.
Kwa
mujibu wa Kiongozi huyo ni kwamba azma ya serikali yaawamu ya tano
kufanya Tanzania kuingia kwenye uchumi wa kati imefanikiwa hivyo ni
jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kwamba mafanikio hayo yanakuwa
endelevu na njia pekee ni kwa kupiga kura na kuwachagua wagombea CCM.
Makange
alisema ipo miradi mkubwa mkoani humo ambayo inapaswa kumalizwa chini
ya Uongozi wa Mgombes Urais wa CCM Dk.John Pombe Magufuli ikiwemo ule wa
ujenzi wa Barabara ya Tanga,Pangani,Saadan mpaka Bagamoyo pamoja na ule
wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka mkoani Tanga.
"Ndugu
zangu njia pekee ya kufanya maendeleo hayo yawe endelevu ni kuchagua
wagombea wa CCM kuanzia Rais,Wabunge na Madiwani....tujitokeze kupiga
kura kwa maslahi mapana ya hatma ya mkoa wetu...",alisisitiza.
Hata
hivyo alisema bado Taifa linahitaji amani na utulivu na chama pekee
ambacho viongozi wake wameienzi amani tangu kupata Uhuru mwaka 1961 ni
CCM pekee.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin