MANYAMA AENDELEA KUMWAGA SERA ACHAGULIWE TENA KILOLELI

Mgombea udiwani kata ya Kiloleli wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Edward Manyama kupitia Chama Cha Mapinduzi akiomba kura kwa wananchi.

Na Suzy Luhende,Shinyanga

MGOMBEA udiwani kata ya Kiloleli wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Edward Manyama kupitia Chama Cha Mapinduzi amewaomba wananchi wa kata hiyo wamchague ili aweze kuendeleza pale alipoishia, ikiwemo kuwapelekea maji ya ziwa victoria, na barabara ambayo ni changamoto kubwa katika kata hiyo.

Manyama amesema hayo wakati akiwa kwenye mkutano wake wa hadhara wa kunadi sera zake katika kijiji na kata ya Kiloleli wilayani humo, ambapo amesema  mambo mengi ya kimaendeleo ameyafanya wakati akiwa diwani miaka mitano,  hivyo anawaomba tena ridhaa wananchi wamchague ili aweze kuendeleza maendeleo pale alipoishia.

Amesema akiwa diwani ndani ya miaka mitano amepambania kuchimba mabwawa ya kunyweshea mifugo, barabara zikatengenezwa ambazo zilikuwa hazipitiki lakini kwa sasa zinapitika, lakini pia zinahitaji kukarabatiwa tena kutokana na mvua kunyesha na kuziharibu.

    "Naombeni sana ndugu zangu mnipe kura zenu zote ili niweze kuwatumikia na kuwaletea maendeleo hamtajutia kunichagua mnanijua ni mchapa kazi mzuri, nitaendeleza mtindo huo ili kuhakikisha kata yetu inapata maji inakuwa na barabara za kupitika vizuri hata wakati wa mvua",amesema Manyama.

Kwa upande wake Underson Mandia  mgombea udiwani kata ya Ukenyenge Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mlezi wa kata ya Kiloleli amesema Manyama ni mpiganaji mzuri wa maendeleo hivyo amewaomba wamchague ili aweze kuendeleza pale alipoishia.

"Ndugu zangu wapendwa tusidanganyike tukachagua upinzani tumchagueni diwani wa kutoka CCM ili aweze kuwapigani namjua ni mpiganaji mzuri hapa kulikuwa na shida ya barabara alipigania mpaka barabara ikachongwa"amesema Mandia" amesema Mandia.

Naye Richard Sangisangi ambaye ni diwani mstaafu wa kata ya Bunambiyu aliwaomba wananchi wa kata ya Kiloleli  kumchagua mgombea udiwani wasishawishike, kuchagua vyama vingine kwa sababu anaweza kuwawakilisha na kuwatoa hapo walipo na kufanya maendeleo makubwa zaidi katika kata.

"Hakuna mwingine wa kufanya maendeleo katika kata hii huyu ndiye jembe tunamjua anajua kushawishi, kwa kuwatetea wananchi wake, hakuna mwingie anayeiweza hii kata"amesema Sangisangi.
Mgombea udiwani Edward Manyama akiomba kura
Mgombea udiwani kata ya Ukenyenge Underson Mandia akiwaombea kura diwani wa kata ya Kiloleli, mgombea ubunge Boniphace Butondo na Mgombea Urais John Pombe Magufuli
Mgombea udiwani Edward Manyama akifurahia wakati akiomba kura
Mgombea udiwani Edward Manyama akimtambulisha mke wake kwenye mkutano wa hadhara wa kunadi sera zake
Aliyekuwa Diwani wa kata ya Bunambiyu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Richard Sangi Sangi akiwaombea kura wagombea wa CCM diwani Edward Manyama, mbunge Boniphace Butondo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kiloleli wilayani Kishapu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post