MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na vikundi vya wanawake katika Kata tatu kwenye Jimbo la Bukoba Mjini MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira katikati (aliyevaa nguo za CCM na miwani) akiwa kwenye picha ya pamoja na vikundi vya wanawake katika Kata tatu kwenye Jimbo la Bukoba Mjini MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akizungumza na wavuvi ambao hawapo pichani kuhusu namna watakavyoweza kunufaika kupitia sekta hiyo
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akizungumza na wavuvi ambao hawapo pichani kuhusu namna watakavyoweza kunufaika kupitia sekta hiyo
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akiwa kwenye picha ufukweni mara baada ya kuzungumza na wavuvi
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kulia akiangalia ng'ombe wanaofugwa wakati alipokutana na wafugaji
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kulia akiteta jambo na mmoja wa wafugaji wakati alipowatembelea ili kubaini changamoto ambazo wanakabiliana nazo na kuona namna ya kuzifanyia kazi
NA MWANDISHI WETU,BUKOBA
MBUNGE
Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania
Bara Neema Lugangira ameahidi kwa kuanzia kuwawezesha kiuchumi vikundi
vya wanawake katika Kata tatu kwenye Jimbo la Bukoba Mjini
Neema
ambaye pia ni Mlezi wa CCM kwenye Uchaguzi huu 2020 kwa Kata hizo
Bukoba Mjini aliyasema hayo mara baada ya kutembelea Vikundi vya Kata za
Kahororo, Nshambya na Kashai ambapo pia walikubaliana vipaumbele vya
uwezeshwaji kiuchumi kwa wanawake wa Manispaa kulingana na Ilani ya CCM
ya mwaka 2020-2025 inavyosema.
Alisema
kwamba lazima vikundi hivyo vitambue fursa zilizopo za uwezeshwaji
wamawake kiuchumi kupitia njia mbalimbali ikiwemo mikopo isiyokuwa na
riba au riba nafuu sambamba na fursa za elimu ya biashara.
“Lakini
pia katika kukutana nao ni kujua kama vikundi vyao vipo hai,
vimesajiliwa, changamoto zao za kupata mikopo na namna ya wao kuweza
kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kuweza kupata mafanikio" Alisema
Hata
hivyo pia Mbunge huyo Mteule amekutana na makundi ya wakulima na
wafugaji wa Kata hizo pia; Kahororo, Nshambya na Kashai mitano kwa lengo
likiwa kupokea changamoto zao ambazo zinawakabili na wakajadiliana kwa
kina na kuzipatia ufumbuzi papo hapo kupitia Ilani ya CCM ya Mwaka
2020-2025.
“Lakini
pia nimewafuata wavuvi walipo kisiwani na kujadiliana nao kuhusu
mageuzi makubwa ambayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) inakwenda kufanya
kwenye Sekta ya Uvuvi itakayopelekea wavuvi wadogo kunufaika zaidi na
sekta yao kama ilivyo kwa wachimbaji madini wadogo" Alisema