POLISI Mwanza wanachunguza chanzo cha kifo cha Deogratias Meded (42) Mkazi wa Sengerema aliyefariki dunia muda mfupi baada ya kudaiwa kula makande na chai akiwa kwenye kampeni za mgombea ubunge jimbo la Sengerema kwa tiketi ya CCM, Hamis Tabasamu ambapo Marehemu alikuwa Meneja wa Kampeni wake.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kifo cha Medard, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema, tukio hilo lilitokea majira ya saa 12:35 jioni katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema .
Alisema marehemu ambaye ni meneja kampeni wa mgombea wa CCM kwnye Jimbo la Sengerema Hamis Mwagao Tabasamu, kabla ya kufikwa na mauti alilalamika kuumwa tumbo baada ya kula chakula (makandekwa chai) na akalazimika kukimbizwa hospitali lakini alipoteza maisha kabla ya kupata tiba.
Muliro alisema kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo hicho kama kimesababishwa na sumu na ni sumu aina gani.
Mbali na uchunguzi pia linaendelea na mahoajino na watu kadhaa waliokuwa na marehemu Medard kwenye kampeni kabla ya kifo ili kubaini chanzo halisi cha kilichosababisha meneja kampeni huyo wa mgombea wa CCM.
Aidha jeshi hilo mkoani humu limesema limejipanga vizuri kuelekea uchaguzi mkuu na kuwataka wananchi wajitokeze kupiga kura Oktoba 28, bila hofu.
Social Plugin