Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BARIADI MHANDISI ANDREA KUNDO AAHIDI KUMALIZA CHANGAMOTO YA TEMBO KUVAMIA MAKAZI

Samirah Yusuph,Mwananchi
Bariadi, Mgombea ubunge jimbo la Bariadi Mhandisi Andrea Kundo, Ameahidi kumaliza kero ya wanyama( tembo ) kuvamia makazi ya wakazi wa kata ya Gilya na Gibeshi katika wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Mhandisi Kundo aliyasema hayo jana alipo kuwa katika mkutano wa kuomba kura kwa wananchi wa kata hizo na kusema kuwa changamoto ya Tembo kuvamia makazi imakuwa ni ya muda sasa hivyo ni muda muafaka kuweza kuimaliza.

Aliongeza kuwa licha ya uwepo wa juhudi za kuhakikisha tembo hao hawaingii kwenye makazi lakini inabidi kuongeza nguvu ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama muda wote.

"Kumekuwa na tembo ambao wamekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi sababu wanaharibu mazao wakati wa mavuno na hata kusababisha vifo, hivyo nitahakikisha magari ya doria za polisi yanakuwa mengi maeneo haya ili tembo waweze kudhibitiwa kuingia katika makazi," alisema Mhandisi Kundo.

Jambo ambalo wananchi wa kata hizo wamelitaja kuwa ni licha ya uwepo wa changamoto zingine lakini hilo ni tatizo kubwa zaidi kwani uvamizi wa wanyama hao kwenye makazi unawaachia balaa la njaa.

Hali inayopelekea mazao yao wanayo vuna kutoka mashambani kwenda kuyahifadhi vijiji vya nkololo na Ihusi umbali wa zaidi ya kilometa 15 ili kuwakepa wanyama hao kwani wanapoingia vijijini wanavunja nyumba na kula mazao yote wanayoyakuta.

Hivyo njia hiyo ya kuhifadhi vijiji vya jirani inafanya mazao yabaki salama lakini changamoto inakuja pale wanapohitaji chakula kutokana na umbali uliopo kwenda kuvifata vyakula vyao kwa ajili ya familia zao.

"Tembo anapo vamia kwenye kaya anabomoa nyumba na anakula chakula chote anachokikuta wanakula michembe, mahindi hata unga na ni ngumu kwafukuza na wengine ni wabishi akigoma kuondoka inabidi wewe ndiye umkimbie," Alisema Monwa Kilatu mkazi wa kata Ihula.

Kwandu Maluguabili alieleza hali anayokutana nayo wanyama hao wanapofika katika makazi yake "Nyumbani nilipoweka mahindi huwa wanakuja kubomoa nyumba wanakula chakula na kuharibu kila wanachokutana nacho lakini baada ya kuwa hatuna chakula hatupati msaada wowote hivyo tunabaki bila chakula".

Wahanga hao walisema kuwa wanahitaji msaada wa serikali ili kuweza kuwadhibiti wanyama hao kwa sababu juhudi zao zinagonga amwamba kutokana na namna ambavyo wamekuwa wakiwafukuza kienyeji hali inayosababisha mapambano kati yao na kusababisha vifo kwa baadhi ya vijana wao.

Tangu mwaka 2017 tembo walinza kupita katika vijiji vya kata hizi wakiwa wanatafuta njia, na tangu waka 2018 wanyama hawa walianza kuvamia makazi nyakati za usiku na kufanya uharibifu katika makazi.

Mwisho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com