Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza, amemtangaza Mwana Fa wa CCM kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya ubunge wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 47,578 na kumshinda Yosepher Komba wa CHADEMA aliyepata kura 12,034.
Mwana Fa anakuwa miongoni mwa wasanii waliofanikiwa kuingia bungeni ambapo wasanii wengine ambao waliingia Bungeni kama Joseph Mbilinyi aliyeshindwa kutetea nafasi yake ya Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini na Joseph Haule ‘Prof Jay’ aliyeshindwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Mikumi.
Social Plugin