Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba (MB) akizungumza na Watumishi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakati wa ziara yake |
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Tume ya taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali akimweleza jambo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa mwaka 2020 hadi 2025
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Tume ya taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali akimkaribisha Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba (MB) katika Ofisi za Tume jijini Dodoma. Wakati wa ziara yake ya kuwatembelea na kuzungumza na watumishi wa Tume Makao Makuu na Watumishi wa Tume mkoa wa Dodoma.
NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba amewataka watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Makao Makuu kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kutimiza azma ya serikali kusogeza huduma muhimu kwa wananchi ikiwemo miundombinu bora ya umwagiliaji kwa wakulima
Mgumba aliyasema hayo leo wakati wa ziara ya kutembelea na kuzungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Makao Makuu na Watumishi wa Mkoa wa Dodoma alisema suala hilo ni muhimu kwa wakulima hatua ambayo itawawesha kuinua vipato vyao na Taifa kwa ujumla.
Alisema pia kuhakikisha wanakuwa tayari kwa jukumu kubwa la kujenga na kusimamia miradi ili iweze kuleta tija kwa maendeleo ya wakulima na jamii nzima
“Kwa kweli niwapongeze watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kupata hati safi na lakini niwatake muendelee kufanya kazi kwa bidii na weledi”Alisema
Awali akizungumza Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali, akimweleza Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa mwaka 2020 hadi 2025 kwa kueleza imejipanga kutekeleza mipango ya serikali ya kukarabati na kujenga Skimu Mpya.
Alisema pia mipango mengine ni kuratibu mipango ya tozo katika Skimu za Umwagiliaji sanjari na kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira na kuhakikisha nchi inavuka kiwango cha uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kutoka asilimia 24 za sasa hadi kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2025 ambapo pia eneo la Umwagiliaji litaongezwa kutoka Hekta 694,715 hadi Hekta 1,200,000.
Social Plugin