Mwanasheria Jenesia Mavere wakati akizungumza kwenye mafunzo kwa wasaidizi wa Kisheria kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Kishapu yenye lengo la kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’ wametakiwa kuwashauri wateja wao kupeleka kwenye mabaraza ya usuluhishi ya migogoro ya ndoa ya kata,Kanisani au BAKWATA migogoro yao ya ndoa kwani Sheria ya ndoa Namba 29 kama ilivyofanyiwa Marekebisho inaelekeza migogoro yote ya ndoa ipelekwe katika mabaraza hayo ya usuluhishi.
Ushauri huo umetolewa leo Jumatatu Oktoba 5,2020 na Mwanasheria Jenesia Mavere wakati akizungumza kwenye mafunzo kwa wasaidizi wa Kisheria kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Kishapu yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),UNFPA na KOICA na kuratibiwa na PACESHI kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia yaliyofanyika Mjini Shinyanga.
Mavere alisema Mabaraza ya usuluhishi ya kata,Kanisa na BAKWATA ndiyo sehemu sahihi ya kupeleka migogoro ya ndoa na endapo usuluhishi katika mabaraza hayo utashindikana basi Baraza litajaza Fomu Namba 3 ambayo itapelekwa mahakamani kwa ajili ya kufungua shauri la mgogoro wa ndoa.
“Ndugu zangu Wasaidizi wa Kisheria naomba niwakumbushe kuwa Mabaraza ya Usuluhishi hayana mamlaka ya kutoa hukumu,kutoa talaka wala kugawa mali za Wadaawa ‘mdai na mdaiwa’ hivyo ni vyema mkawa makini pindi wateja wanapowaletea kesi za migogoro ya ndoa”,alisema Mwanasheria Mavere.
Kwa upande wake, Wakili Neema Ahmed aliwakumbusha Wasaidizi wa Kisheria kutojihusisha na usuluhishi wala upatanishi wa migogoro ya kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia kama vile vipigo na ukatili wa kingono kwani yanaingia katika makosa ya jinai.
“Wasaidizi wa kisheria na wananchi kwa ujumla panapotokea kesi za jinai mnatakiwa kuzipeleka kwenye madawati ya jinsia polisi au kwa walinzi wa amani kwenye maeneo husika (maafisa watendaji wa kata na vijiji)”,alisema Wakili huyo.
"Tusisitize pia malezi shirikishi ya watoto baina ya baba na mama. Kesi zinazohusu matunzo ya watoto zipelekwe kwenye mahakama za watoto", aliongeza Neema.
Mwanasheria Jenesia Mavere wakati akizungumza kwenye mafunzo kwa wasaidizi wa Kisheria kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Kishapu yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),UNFPA na KOICA na kuratibiwa na PACESHI kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia katika ukumbi wa Shinyanga Fairies Hotel Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Mwanasheria Jenesia Mavere akitoa mada ya Ndoa kwenye mafunzo kwa wasaidizi wa Kisheria yaliyolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Mwanasheria Jenesia Mavere akiendelea kutoa mada kwenye mafunzo kwa wasaidizi wa Kisheria yaliyolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Mwanasheria Jenesia Mavere akiwasisitiza Wasaidizi wa Kisheria ‘Paralegals’ kuwashauri wateja wao kupeleka kwenye mabaraza ya usuluhishi ya migogoro ya ndoa ya kata,Kanisani au BAKWATA migogoro yao ndoa kwani sheria ya ndoa Namba 29 kama ilivyofanyiwa Marekebisho inaelekeza migogoro yote ya ndoa ipelekwe katika mabaraza hayo ya usuluhishi.
Wakili Neema Ahmed akiwakumbusha Wasaidizi wa Kisheria kutojihusisha na usuluhishi wala upatanishi wa migogoro ya kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia kama vile vipigo na ukatili wa kingono kwani yanaingia katika makosa ya jinai.
Wakili Neema Ahmed akiwasisitiza Wasaidizi wa Kisheria kupeleka kesi za jinai kwenye madawati ya jinsia polisi au kwa walinzi wa amani kwenye maeneo husika na kesi zinazohusu matunzo ya watoto zipelekwe kwenye mahakama za watoto.
Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Kishapu/ Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), wilaya ya Kishapu, Mwajuma Abeid akitoa mada kuhusu MTAKUWWA.
Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Kishapu/ Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA),wilaya ya Kishapu, Mwajuma Abeid akitoa mada kuhusu MTAKUWWA.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin