Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAHABUSU ALIYEKUWA AKIKABILIWA NA KESI YA MAUAJI AMEFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA RADI GEREZANI


Mahabusu Mussa Hajji Mshana (25), aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji, amefariki dunia katika Gereza la Wilaya la Mng’alu Kibiti baada ya kupigwa na radi, huku wengine wanne wakijeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi majira ya saa sita mchana katika gereza hilo.

Aliwataja waliojeruhiwa ni mfungwa Richard Mai (24) mfungwa namba 37/2020, Hashim Rashid (26) namba 154/2020, Ismail Mtupa namba 155/2020 na Issa Hajji (21) namba 31/2020, ambao wanaendelea na matibabu katika Kituo cha Afya Ikwiriri.

Alitoa wito kwa wananchi kanda maalum ya Kibiti, Rufiji, Mafia na Mkuranga kuchukua tahadhari wakati wa kipindi chote cha mvua za vuli zinazoendelea kunyesha nchini.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, hakuna mahabusu wala mfungwa aliyekimbia kufuatia tukio hilo, na kwamba ulinzi na usalama vimeimarishwa kanda yote ya mkoa wa kipolisi Rufiji. 

Credit: Nipashe




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com