Rais wa Marekani Donald Trump jana amepelekwa katika hospitali ya kijeshi kupatiwa matibabu baada ya kukutikana na ugonjwa wa Corona.
Trump amehamishiwa katika hospitali ya Walter Reed saa 17 baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa huo.
Katika vidio fupi aliyoituma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Trump ameonekana akisema kwamba hali yake inaendelea vizuri.
Msemaji wa Ikulu ya White House Kayleigh McEnany amesema Trump atafanya kazi katika chumba maalum hospitalini kwa siku chache zijazo kama hatua ya tahadhari.
Inasemekana kwamba Trump mwenye umri wa miaka 74, anasumbuliwa na homa na kwamba atapewa dawa ambayo bado inafanyiwa majaribio.
Rais huyo wa Marekani wa chama cha Republican amepata ugonjwa wa Corona akiwa katikati ya kampeni kuelekea uchaguzi wa mwezi Novemba ambapo atachuana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden.
-DW
Social Plugin