Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge mapema leo amepiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Kawe “A” ambapo baada ya kupiga kura amezungumza na wanahabari na kuwataka wananchi wa mkoa wake kujitokeza kupiga kura kwani hadi sasa hakuna tukio lolote ambalo limeripotiwa la uvunjifu wa amani na hivyo Dar es Salaam ipo Shwari licha ya changamoto ndogondogo ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi inazishughulikia ili kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura apate haki yake ya msingi ya kikatiba.
Social Plugin