RC NCHIMBI: TUTACHUKUA HATUA KWA YEYOTE ATAKAYE HATARISHA AMANI YA NCHI

 

Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi  akihutubia wananchi, wazazi na wanafunzi wakati wa sherehe za mahafali ya kuhitimu kidato cha nne kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari.Mandewa wanaosali  Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC), mkoani hapa jana. 

Wanafunzi, wananchi na wazazi wakiwa kwenye mahafali hayo. 
Wananchi na wazazi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.
Watoto wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wake wa wachungaji wa kanisa hilo wakiwa kwenye mahafali hayo.
Askofu wa kanisa hilo, Gasper Mdimi (kushoto) Mchungaji Abeli Manupa na Mwalimu Mkwiye Emmanuel (kulia) wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.
Wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti Mhitimu, Faraja Nyambi.
Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti Mhitimu, Betha Isaya.
Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti Mhitimu, Alex Stephano.
Mahafali yakiendelea.
Wahitimu hao wakiombewa.
Mgeni rasmi Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi na  viongozi wa kanisa hilo wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao. 

 Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi na viongozi wa kanisa hilo wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kiislamu waliofika kanisani hapo kushiriki na wenzao kwenye mahafali hayo. 


Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi amesema serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayehatarisha amani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. 

Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyasema hayo alipohutubia wananchi, wazazi na wanafunzi wakati wa sherehe za mahafali ya kuhitimu kidato cha nne kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mandewa wanaosali Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC), mjini Singida jana. 

"Kuna watu fulani fulani wanazungumza maneno yenye kila aina ya viashiria vya uvunjifu wa amani wakidhani huenda kipindi hiki cha kampeni serikali haipo kazini. Niwatahadharishe kamwe wasithubutu kufanya hivyo wataishia kwenye mkono wa sheria," alisema na kuongeza:"Mpaka mda huu serikali ipo, na Rais wetu sote bado ni Dk. John Pombe Magufuli. 

Katika hatua nyingine, 'Mama' Nchimbi alimpongeza Rais kwa ujasiri,na maono yake kwa namna ya pekee alipofanikiwa kulivusha salama Taifa dhidi ya janga hatari la Corona.

"Haya maamuzi sio mepesi mepesi tazameni nchi nyingine zinavyoendelea kuteseka mpka sasa...kwakweli tunamshukuru sana Rais na Mwenyezi Mungu aendelee kumuongoza na kumjalia hekima na busara ili mapenzi yake ya dhati kwa watanzania wenzake yazidi kushamiri." 

Aidha, katika mahafali hayo yaliyofanyika kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC), Nchimbi aliwakumbusha wazazi kuepuka kuwapa simu watoto wawapo masomoni ili kuwajengea nidhamu ambayo itakuwa ni msingi wa ufaulu na mafanikio yao kwenye tafakari ya masomo. 

Akizungumzia maisha ya wahitimu hao baada ya kidato cha nne, aliwaasa kuwa waangalifu na kuepuka mitego na vishawishi vya kidunia ambavyo vinaweza kuwatumbukiza katika mashimo ya dhambi na kuharibikiwa, ikiwemo kupoteza ndoto zao njema za maisha walizonazo. 

Kwa upande wake, Askofu wa kanisa hilo, Gasper Mdimi aliwataka wahitimu hao kutafakari sambamba na kuchukulia mahafali hayo na malezi waliyopewa kwa kipindi chote kama kiapo chao kwa Mungu cha kutotenda dhambi wala kurudia kutenda dhambi na wasisahau kila mmoja kuendelea kulinda usafi wa moyo popote pale watakapokuwepo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post