TANAPA WATOA TAARIFA MOTO UNAOWAKA MLIMA KILIMANJARO

Mlima Kilimanjaro uliopo nchini Tanzania ambao ni Mlima mrefu zaidi barani Afrika unawaka moto.

Taarifa ya shirika la hifadhi za taifa Tanzania TANAPA iliyotolewa na kamishna msaidizi Mwandamizi kitengo cha Mawasiliano TANAPA Paschal Shelutete, inaeleza kuwa moto huo umezuka kutokea eneo la Whona ambacho ni kituo cha kupumzikia wageni wanaopanda mlima Kilimanjaro kupitia njia ya Mandara na Horombo. 

Shelutete amesema miale ya moto ilianza kuonekana siku ya Jumapili mchana kutoka mji wa Moshi kaskazini mwa Tanzania, kilometa zaidi ya 20 kutokea eneo la mlima kulitotokea moto huo. 

Amesema Mpaka sasa juhudi za kuuzima moto huo bado zinaendelea huku akibainisha kuwa vikosi vinavyoshiriki katika kuudhibiti moto huo vinajumuisha wananchi, wanafunzi wa mafunzo kwa vitendo na wale wa Chuo cha Mweka na Kikosi cha Zimamoto. 

Kuhusu chanzo cha moto huo mamlaka hiyo, amesema bado inaendelea kufanyia taarifa mbalimbali ilizozipata. 

Amesema wanaendelea kuchukua tahadhari zote kuhakikisha usalama wa wageni na vifaa vyao unaimarika bila kuathiri shughuli za utalii ambazo zinaendelea kama kawaida hususani kwa njia ya Marangu iliyoathirika na moto huo.


 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post