Akizungumza katika Mkutano huo mwakilishi kutoka Tigo Tanzania ambaye pia Ni Mkuu wa kitengo cha huduma za kifedha biashara na mahusiano Bi. Faith Pella ameipongeza serikali kwa juhudi kubwa inayofanya kuziunga mkono Taasisi binafsi hasa kwa upande wa huduma za Kimtandao maana kupitia mashirika yake kama vile TANESCO, DAWASCO n.k ambapo Sasa mtu anaweza kulipia kodi , bili na madeni mbalimbali Kidigitali kupitia simu ya mkononi
"Najivunia sana kuhusu nchi yangu na SERIKALI yangu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu wao ndio namba moja kwenye kutangaza na kusukuma Maendeleo ya Kidigitali hapa nchini , ukiangalia huduma nyingi za kiserikali zimeunganishwa moja kwa moja na malipo kwa huduma za Kimtandao " alisema Bi. Faith Pella.
Aidha kwa upande mwingine amesema Tigo imekua kinara katika utoaji wa fursa kwa vijana kupitia huduma zake mbalimbali na kuongezea kuwa bado nafasi zipo kwa vijana kuweza kujipatia kipato kupitia Uwakala wa Tigo Pesa na huduma nyingine mbalimbali zinazotolewa na Kampuni iyo namba moja Nchini.
Mkutano huo unaendelea kwa siku tatu Mfululizo na leo ilikua ni siku ya Pili katika Ukumbi wa JNICC uliopo Posta Jijini Dar es Salaam.
Social Plugin