Dar es Salaam, 21 October 2020: Kampu
Mkumbo Myonga, Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano kutoka Tigo Tanzania, amesema, “Ushirikiano wetu na Transsion Holdings tunaubeba kwa fahari kubwa kwa sababu unaenda sambamba na dira yetu ya kuhakikisha tunatoa huduma bora za kisasa kwa wateja wetu wote. Uzinduzi huu wa leo, ni wa simu nyigine ya kisasa kabisa na ya gharama nafuu ni udhibitisho kwamba kama kampuni tumejidhatiti kuhakiksha kila mteja wetu anafurahia matunda ya vifaa hivi vipya vya kisasa ambavyo vimeunganishwa na huduma bora za kidigitali zinazotolewa na Tigo”.
“Tuko hapa leo kuendelea kutimiza ahadi zetu kwa watanzania za kuhakikisha kila raia anafurahia kutumia simu janja za kisasa huku akiwa ameunganishwa na mtandao wa 4G ulionenea kote nchini. Simu hizi mpya zinapatikana sasa katika maduka yetu yote nchi nzima. Pia ikumbukwe kuwa simu hii ya ITEL T20 inakuja ikiwa na ofa ya GB 30 za intaneti ambazo zitatumika kwa mwaka mzima. ITEL T20 ni simu mpya yenye huduma za kisasa za simu janja zenye uwezo wa 4G na itakuwa inapatikana kwa kiasi cha shilingi 84,900/- tu”, Myonga ameeleza.
Afisa Uhusiano Kutoka ITEL,Fernando Wolle, amefurahishwa na ubia huo na Tigo Tanzania katika uzinduzi wa simu janja ya ITEL T20. “Tumeingia ubia huu na Tigo ili kuongeza thamani ya simu yetu. ITEL T20 ni zaidi ya simu janja nyingine kwa sababu imewekwa huduma nyingi za kidigitali. ITEL T20 ni simu janja yenye uwezo wa 4G ikiwa na ukubwa wa screen wa nchi tano na uwezo wa 1GB+16GB huku ikiwa inafanya kazi kwa kutumia mfumo mpya wa Android P Go edition OS. Jina T20 linawakilisha, T= Tigon a 20 inawakilisha mwaka 202”, amesema Wolle.
ANGALIA TUKIO ZIMA HAPA
Social Plugin