Mwenyekiti wa Tume ya Taifa (NEC) Jaji Semistocles Kaijage ameonya vikali taasisi, watu au vikundi vya watu waliojipanga kutangaza matokeo ya uchaguzi baada ya zoezi la upigaji wa kura Oktoba 28 kwa kufanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi mkuu kwa mujibu wa katiba ya nchi.
Kauli hiyo ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi anaitoa zikiwa zimebakia siku nane kuelekea katika uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani na kubainisha jukumu la kutangaza washindi wa uchaguzi ni tume ya taifa pekee na sio vinginevyo.
Kadhalika mwenyekiti huo wa uchaguzi akatangaza zoezi la kuanza kutoa vitambulisho kwa mawakala walioteuliwa na vyama vya siasa kuanzia oktoba 21
Social Plugin