BALOZI wa China Wang Ke akiwa anasisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira
BALOZI China Wang Ke na Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira wakikabidhiana makubaliano ya ushirikiano waliyoyasaini leo Octoba 14,2020
BALOZI wa China Wang Ke na Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira wakionyesha makubaliano ya ushirikiano baina ya Ubalozi wa China na Agri Thamani Foundation
UBALOZI wa China umeingia Makubaliano ya Kushirikiana na
Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation katika
maeneo ya afya, elimu na kilimo kwa wanawake na mabinti hapa nchini.
Akizungumza
wakati wa utiliaji saini makubaliano hayo yaliyofanyika Ubalozi wa
Chini Jijini Dar es Saaalm Balozi wa chini nchini Wang Ke alisema
ubalozi huo upo tayari kuchangia maendeleo ya jamii kwa wanawake na
mabinti kutoka mikoani/vijijini na imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
Alisema
kwamba Octoba 11 mwaka huu ilikuwa ni Siku ya Watoto wa Kike Duniani
hivyo katika kuenzi siku hiyo katika makubaliano yaliyosainiwa leo
Ubalozi huo umetoa msaada kwa Agri Thamani wa kununua taulo za kike kwa
ajili wanafunzi wa sekondari wa kike 1,500.
Balozi
huyo alisema taulo hizo za kike zitapelekwa kwenye Mikoa ya Kagera,
Geita, Kigoma, Tabora, Tanga, Dodoma na Lindi ambapo watoto hao wa kike
watatoka kwenye familia zenye uhitaji mkubwa zaidi na watapata msaada
huu kwa kipindi cha mwaka mzima ili masomo yao yasiathirike.
Aidha
pia balozi alisema mkataba huu umesainiwa leo siku ya Nyerere ikiwa pia
ni sehemu ya kumuenzi maana aliwahi kusema Tanzania itapambana na adui
wakubwa watatu katika maeneo ya elimu, umaskini na afya .
“Mkataba
huu ambao Ubalozi wa China na Agri Thamani imesaini leo tarehe
14/10/2020 ni jitihada za kuendelea kuenzi maneno ya Nyerere na kuyaishi
kwa vitendo lakini pia kudhihirisha ushirikiano mkubwa baina ya China
na Tanzania”Alisema Balozi huyo.
Awali
akizungumza wakati wa makubaliano hayo Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa
la Kiserikali la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira alianza
kumshukuru Balozi Wang Ke kwa utayari wake wa kushirikiana na Agri
Thamani huku akieleza huo ndio utakuwa mwanzo na wamejipanga
kushirikiana katika maeneo mahsusi yatakayopelekea kumuinua mwanamke
kiuchumi kwani ukimwezesha mwanamke na mtoto wa kike utakuwa umeiwezesha
jamii nzima.
Aidha
alisema Shirika hilo la Agri Thamani linatoa elimu ya Lishe kwenye
Shule za Sekondari na Masuala ya Hedhi Salama na Afya ya Binti ikiwa ni
sehemu ya Lishe Bora hivyo anaamini kuwa msaada huu wa taulo za kike kwa
wanafunzi wa sekondari 1,500 utakuwa msaada mkubwa sana kwa mabinti
hawa hususan kwa wale ambao watakuwa kwenye mwaka wa mitihani ikiwemo
Kidato cha 2 na cha 4 ambao ndio walengwa.
Hata
hivyo alisema kwamba ni matarajio yao kuwa mpango huo utakuwa endelevu
ili iweze kufikia wanafunzi wa kike wengi zaidi kwa kutumia ubunifu na
teknolojia mbalimbali kuhakikisha wanaondokana na changamoto ya
kukosekana kwake.
Social Plugin