MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Majengo Salim Perembo wakati wa mkutano wa Ummy wa kampeni uliofanyika uwanja wa Lamore Jijini Tanga
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa Kata ya Majengo kwenye uwanja wa Lamore Jijini Tanga
Msanii wa Mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza wakati mkutano huo wa kampeni
Msanii wa Mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza wakati mkutano huo wa kampeni WANANCHI wa Kata ya Majengo wakiwa kwenye mkutano wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
WANANCHI wa Kata ya Majengo wakiwa kwenye mkutano wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu WANANCHI wa Kata ya Majengo wakiwa kwenye mkutano wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema atahimiza uwekezaji ili kuwezesha ujenzi wa viwanda vipya kwenye Jiji la Tanga ikiwemo vile kuvifufua vya zamani ili kuongeza fursa za ajira na vipato kwa wananchi.
Ummy
ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Majengo Jijini Tanga
wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika uwanja wa Lamore.
Alisema
endapo wananchi watamchague hawataweza kujutia kutokana na mipango mizuri
aliyonayo kuhakikisha wanawake, vijana na wanaume wanaweza kuinuka kiuchumi na
hivyo kuweza kuongeza vipato vyao.
“Binafsi
ninaamini endapo tutakuwa na viwanda Tanga itachangamka vijana, wakina mama na
wanaume watapata ajira na hivyo kuchochea kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi kwenye
Jiji la Tanga “Alisema
Aidha
alisema mkakati wa pili ambao utawezesha kuwajaza manoti wakazi wa Tanga ni kupigania
maboresho ya awamu ya pili ya bandari ya Tanga ili kufungua furza za kiuchumi
na kipato kwa wana Tanga.
“Mkakati
wangu wa tatu ni kuhakikisha ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini
Uganda hadi Chongoleani Tanga unakamilika na katika hili namshukuru Rais Dkt
John Magufuli ambaye amewezesha bomba hilo kujengwa kwenye Halmashauri ya Jiji
la Tanga”Alisema
“Hivyo
ninawaomba mnipe kura zenu zote za ndio, wanawake wenzengu naombeni mninyanye
mwanamke mwezengu kwa kunipa kura za ndio ili tukaweke historia jimbo la Tanga
kuongoizwa na mwanamke pia niwaomba mpe kura za ndio Rais Dkt Magufuli
Aliwaomba
wananchi hao wamchague Rais Dkt John Magufuli ili aweze kuendelea kuwa Rais
kazi yake kwenye Jiji la tanga katika kata ya Majengo inaonekana
amewezesha utolewaji elimu bure kwa watoto kwenye kata za Majengo tumpe kura
zetu zote za ndio”Alisema
Ummy
aliwaomba wamchague ili aweze kusimamia suala hilo kwani anauhakika wataweza
kupata ajira nyingi kwa wakazi wa Jiji la Tanga na Kata ya Majengo ikiwemo
kuwawezesha kiuchumi vijana kwa kuwapigania mikopo vijana.
“Katika
kata ya Majengo vijana wengi wanajishuhughulisha na dawa ya kulevya lakini kwa
sababu hawana shughuli za kufanya ninawaomba mnichague ili niweze kuanzisha
program mbalimbali za kuwawezesha vijana kuweza kujiajiri na kufanya shughuli
nyengine za kujiongea vipato”Alisema
Hata
hivyo alisema pia endapo akichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo ataanzisha
ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Majengo ili kuwasaidia watoto wasiende
kwenye shule za mbali.