Na John Walter- Mbulu
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga amesema watahiniwa 3,941 wakiwamo wasichana 2,198 na wavulana 1,743 wanatarajiwa kufanya mitihani ya taifa ya kuhitimu darasa la saba Oktoba 7 hadi 8,2020.
Akizungumza na waandishi wa habari, amesema wanafunzi wote hao wapo tayari kwa ajili ya mtihani huo wa Taifa.
Kamoga amesema kuwa mitihani hiyo itafanyika kwa siku mbili (Jumatano na na alhamisi ) na mpaka sasa taratibu zote zimeshakamilika na serikali imeshatoa fedha zote zinazohitajika kwa ajili ya zoezi hilo.
Amesema wahitimu hao wote ni wanufaika wa matunda ya Elimu bila malipo ambapo serikali katika Halmashauri ya wilaya ya Mbulu ilitoa shilingi Bilioni 4.9 ambazo Bilioni 3.5 zilihudumia Shule za Msingi na Bilioni 1.4 katika Shule za Sekondari tangu mwaka 2016 ilipoanza Elimu ya msingi na Sekondari bila malipo ambapo wanafunzi hao walikuwa darasa la tatu.
Ametoa wito kwa wazazi/walezi kuhakikisha wanawahimiza watoto wao kufika kwa wakati kufanya mtihani huo muhimu na ni kosa kisheria kumzuia mwanafunzi kufanya mtihani.
Social Plugin