Mwakilishi wa katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Charles Mtali akizungumza wakati wa halfa hiyoMwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima Tanzania Makao Makuu Baraka Kionywaki akizungumza wakati wa halfa hiyoMeneja wa Elimu BRAC Maendeleo Tanzania William Manoah akieleza jambo kwa waandishi wa habari wakati wa halfa hiyoMmoja kati ya wanufaika wa mradi huo akitoa ushuhudaMmoja kati ya wanufaika wa mradi huo akitoa ushuhudaSehemu ya wanufaika wa mradi huo wakifuatilia matukio mbalimbali
WANAFUNZI 10 wa kidato cha Sita waliosoma elimu ya Sekondari nje ya mfumo rasmi(Elimu Mbadala ) kupitia mradi wa elimu nje ya mfumo rasmi unaotekelezwa Mkoani Tanga na Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania chini ya ufadhili wa Shirika la Norad wamefanikiwa kupata alama za juu za kuwawezesha kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini.
Mradi wa elimu nje ya mfumo rasmi (Alternative Education Program) unaohusu uwezeshaji wa elimu na stadi za maisha kwa wasichana na watoto ambao unatekelezwa mkoani Tanga na BRAC Maendeleo Tanzania kwa kipindi cha miaka minne toka Juni 2018 hadi Aprili 2022 kupitia ufadhili wa Shirika la NORAD (Taasisi ya ushirikiano wa maendeleo nchini Norway)
Akizungumza wakati wa maafali na halfa ya kuwapongeza wanafunzi hao, Meneja wa Elimu Brac Tanzania William Manoah alisema wamefurahia na wanafunzi waliokuwa wakiwafadhili muda mrefu waliowakuta mitaani waliokosa fursa ya kusoma sekondari waliacha masomo kwa sababu mbalimbali.
Alisema kwamba baada ya kuwapata mitaani waliwasaidia kuwafadhili waweze kusoma sekondari kwa kushirikiana na Serikali kupitia taasisi ya elimu ya watu wazima makao makuu na kupitia mkufunzi mkazi wa elimu Tanga na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ras na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga kuanzisha mradi huo mwaka 2016.
Alisema lengo likiwa kuwakomboa wasichana walioacha shule kwa sababu mbalimbali na serikali inasera ambayo ipo wazi kabisa mtu aliysehindwa kuendelea na shule kupitia mfumo rasmi anafursa ya kusoma nje ya mfumo rasmi na waliowasaidia walimaliza kidato cha nne na kwenda shule mbalimbali.
Manoah aliongeza kwamba makundi ya leo wasichana wanaowapongeza wapo 10 ambao waliamua kusoma kidato cha sita na wamefaulu kwa alama za juu daraja la kwanza na la pili.
“Tunafurahi kama shirika matunda ambayo tumeyaanzisha kwa kushirikiana na serikali leo tumeyaona waziwazi lakini pia wengine hawakwenda kidato cha tano na sita bali wamekwenda kwenye vyuo vya kati na masomo ya ufundi na makundi yote hayo walishindwa kufika katika elimu kwenye mfumo rasmi “Alisema
“Brac Tanzania tumefurahi kuona kazi tunayoifanya ina matokeo Tanzania na tumewafikia wengi tunawashukuru wafadhili wetu Taasisi ya ushirikiano wa maendeleo nchini Norway (Norad) kwa kutoa fedha za kutusaidia”Alisema
Awali akizungumza katika halfa hiyo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima Tanzania Makao Makuu Baraka Kionywaki alilipongeza shirika la Brac Maendeleo Tanzania kwa jinsi ilivyofanikiwa katika kutoa elimu kwa mabinti hao ni kazi nzuri sana.
Baraka ambaye pia Mratibu wa Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari nchini kwa njia mbadala alisema kazi hiyo imewezesha kuwasaidia vijana wengi kupata elimu ambayo imewawezesha kuweza kujikwamua.
Naye kwa upande wake mgeni rasmi kwenye maafali hayo Mwakilishi wa katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Charles Mtali aliipongeza Shirika la BRAC Tanzania kwa kuwezesha utoaji wa elimu kwa wanafunzi hao huku wakihaidi kuendelea kuwaunga mkono kwenye jitihada zao.
Mtali ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Aidha pia aliwataka wazazi na walezi kuacha kukwepa majukumu ya kifamilia ya kuwalea watoto wao.
Social Plugin