Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANCHI 200,330 WANUFAIKA NA MIRADI YA MAJI SIMIYU


Samirah Yusuph,

Simiyu. Wananchi wa mkoa wa Simiyu wanatarajia kunufaika na miradi ya maji  71 ifikapo desemba mwaka huu katika vijiji 162 ndani ya wilaya zote.

Miradi hiyo iliyo katika hatua mbali mbali za ukamilishaji huku  miradi 35 ikiwa tayari imekamilika na inaendelea kuwanufaisha wananchi wa maeneo na kuwaondolea adha ya uhaba wa maji.

Hali iliyoelezwa na baadhi ya wananchi wa wilaya ya meatu  kuwa kwao ilikuwa ni ndoto kupata maji safi na salama kutokana na ukame uliopo katika maeneo hivyo miradi hiyo imekuwa ni msaada usio weza kuelezeka.

"Kwa sasa hakuna changamoto ya maji katika maeneo yetu, tunakuja kuchota maji kwenye vituo vya maji ya kuhudumia wananchi lakini kwa wale walio na uwezo wamevuta mabomba mpaka majumbani kwa hiyo changamoto ya maji hatuna tena" alieleza Kapongo Mhoja.

Uwepo wa miradi hiyo umewafanya waache kuamka usiku wa manane kwenda mtoni umbali wa kilomita zaidi ya ishirini ili kwenda kutafuta maji ambayo ilikuwa ni ngumu kujitosheleza kwa sababu ya umbali uliokuwepo uliruhusu kupata maji kidogo.

"Tulikuwa tunaenda usiku wa manane na tunarudi jioni na pengine unandoo moja au mbili na hayo maji ukiyafikisha yanatumika yote inabidi tena siku inayofata uende kuyatafuta hivyo muda mwingi tulipoteza kwenye kitafuta maji," alieleza Elizabeth Masungwa.

Hali hiyo ambayo inawafanya wananchi hao kuahidi kuitunza miundombinu ili iendelee kutoa huduma jambo ambalo lilisisitizwa na mkurugenzi msaidizi idara ya rasilimali za maji Pamela Temu amabapo ni jukumu la wananchi kulinda miundo hiyo.

Ambapo alisema kuwa teknolojia iliyotumika katika ujenzi wa miundo mbinu hiyo ni ujenzi wa mabwawa katika mito ili kutengeneza vyanzo ambavyo vitasambaza maji katika mpampu ambazo zinapeleka kwa watumiaji.

"Teknolojia hiyo ni suruhisho la maeneo yenye ukame kwani kutakuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji kwa misimu yote ya mwaka na wananchi watasahau kuhusu changamoto ya maji," alisema Pamela.

Akikagua utekelezaji wa miradi hiyo wilayani meatu jana Mhasibu mkuu wizara ya maji Ahadi Msangi alisema kuwa, wamejionea kazi hiyo ilivyofanyika kwa umahili ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Aliendelea kuwa "Utekelezaji umefanyika kwa kiwango kizuri hivyo nimeridhishwa na utendaji, na kazi kibwa imefanyika hivyo ifikapo desemba miradi yote itakuwa imakamilika na itakwa na manufaa zaidi kwa wananchi,"

Wananchi 529,125 wanatarajiwa kunufaika na miradi hiyo pindi ukamilishaji wa miradi 36 utakapo malizika ifikapo desemba 2020.

Mwisho.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com