Na Allawi Kaboyo – Ngara.
Naibu katibu mkuu wizara ya maji ambaye anaendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maji mkoani Kagera Mhandisi Nadhifa Kemikimba, amesikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wasiokuwa wazalendo kwa nchi yao vya kuhujumu miradi ya maji kwa kuharibu miundombinu na baadae kuanza kulalamika kuwa hawapati huduma ya maji.
Mhandisi Nadhifa ameyasema hayo Okitoba 14, mwaka huu alipofika katika kijiji cha RWINYANA baada ya kupokea malalamiko mbalimbali ya wananchi wa kijiji hicho kuwa hawapati maji na kuamua kwenda kwenye chanzo cha mradi huo ili kuangalia tatizo ni nini kwanini wananchi hawapati maji.
Katika safari hiyo ya kuelekea kkenye chanzo hicho cha maji Naibu katibu mkuu ameambatana na baadhi ya wananchi akiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho pamoja na wataaamu aliokuwanao kwenye msafara, mara baada ya ya kufika kwenye chanzo hicho aliridhika na wingi wa maji unaozalisha ambapo alisikitishwa na vitendo vya wananchi kuanzisha kilimo kwenye chanzo hich na sehemu nyingine kukuta mabomba ya maji yakiwa yamekatwa kwa vitu vyenye ncha kali na kupelekea maji kumwagika kwa kiasi kikubwa.
“Lengo la serikali ni kuhaikisha wananchi wote hasa wa vijijini wanapata huduma ya maji safi, lakini baada ya kufika kwenye mradi huu nimepokea maalamiko ya wananchi kuwa mradi huu hautoi maji na hata yakitoka basi hayakidhi mahitaji huku serikali ikiwa imetumia fedha nyingi kuutekeleza mradi huu, nilichogundua hapa nyote ni mashaihidi nyinyi wananchi ndio sababu mojawapo ya kutopatikana kwa maji ya uhakika katika kijiji chenu, mmeona hapa mabomba yamekatwa kabisa na maji yanamwagika.” Aesema naibu katibu mkuu.
Aidha kufatia hali hiyo amemuagiza mhadishi wa wakala wa maji vijijini RUWASA kuanza ukarabati wa mradi huo ambao unamiaka 7 toka uipoanza kutekelezwa ili uanze kutoa maji ya uhakika kwa wanachi kama ilivyokuwa imekusudiwa kabla ya siku kuku za Krismas za mwaka huu.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo meneja wa RUWASA wilaya ya Ngara MhandisiAbdi Andaru amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 3013 na kutarajiwa kukamiika mwaka 2014 huku gharama za mradi huo zikiwa ni shilingi za kitanzania zaidi ya shingi milioni 501 ambapo mkandarasi aitwaye Nyamasirir General Promotion & Supplies akiwa amelipwa kiasi zaidi ya shilingi milioni 455.
Akiwa katika wilaya za Missenyi, Kyerwa na Karagwe Naibu katibu mkuu alitembelea na kukagua miradi ya maji ya Kijiji BISOLE upande wa Kyerwa na mradi wa CHABUHOLA upande wa wilaya Karagwe ambapo amewaagiza mameneja wa wilaya hizo kuhakikisha wanaibua miradi ambayo itawawezesha wananchi kupata maji kwa ukaribu zaidi kwa kuwa wananchi hao hawajajiskusanya sehemu moja.
Domini Kasigwa ni Mwenyekiti wa kijiji BISOLE ambayye ameeleza kuwa kabla ya ujio wa madi huo walikuwa wakiteseka sana kufata maji mbali na zaidi walikuwa wakitumia maji ya madimbwi hali iliyowapekea kuhatarisha afya zao kutokana na kutumia maji amabayo sio salama , ambapo ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa kuwaletea mradi mkubwa wa maji na sasa wanafuhia maisha.
MWISHO.