Wanne Wahukumiwa Kwa Kuisababishia TCRA Hasara ya Milioni 16
Tuesday, October 13, 2020
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu wafanyabiashara wanne wakiwemo raia wawili wa kigeni kulipa fidia ya shilingi milioni kumi na sita (16) kwa kosa la kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA hasara ya zaidi ya shilingi milioni kumi na sita (16).
Washitakiwa hao ni Alven Swai, Godluck Macha wakazi wa Mbezi beach Jijini Dar es Salaam, wengine ni Betha Ngunyi na Frolennce Wanjira wakazi wa Nairobi Nchini Kenya wamehukumiwa kulipa fidia hiyo baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini DPP.
Katika shauri hilo namba 58 ya mwaka 2020 iliyosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Yusto Ruboroga, washitakiwa Betha Ngunyi na Frolennce Wanjira wametakiwa pia kulipa faini Shilingi laki tano kila mmoja kwa kosa la kuishi nchini bila vibali maalumu vinavyotambulika kisheria.
Hata hivyo washitakiwa hao wamefanikiwa kulipa faini hiyo baada ya kufikia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini DPP kukiri makosa yao.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin