Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATU 15 WAFARIKI KWA AJALI, NGARA – KAGERA BAADA YA BASI LA EMIRATES KUPINDUKA

Watu  15 wamefariki dunia na wengine 18 wamejeruhiwa mkoani Kagera kufuatia ajali ya basi la Emirates ambalo hufanya safari zake kati ya Ngara na Mwanza.


Ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo kuanguka na majeruhi wamelazwa Hospitali Teule ya Nyamiaga wilayani Ngara leo Jumamosi, Oktoba 24, 2020.

Mkuu wa wilaya Ngara, Michael Mntenjele, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema: “Ni kweli ajali hiyo imetokea mbele kidogo kutoka hapa Ngara mjini..Eneo la tukio kuna mteremko mkali, huenda gari lilimshinda breki, kwa hiyo akawa amepata ajali na kuanguka upande wa mteremko.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com