Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa akifunga Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit).
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe amewataka Wataalamu wa Afya nchini kuwajibika katika maeneo yao ili kuboresha huduma za afya,ustawi wa jamii na lishe nchini
Dk. Kapologwe ametoa wito huo leo Alhamis Novemba 26, 2020 Jijini Dodoma wakati akifunga Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit) lililoshirikisha wadau wa sekta ya Afya kutoka taasisi za Umma, Mashirika ya dini na binafsi kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya afya nchini.
Amesema ili kuboresha huduma za afya,ni lazima kila mtu awajibike katika eneo lake na kwamba kama kila mtu atawajibika atachangia pato la nchi.
“Huu ni muda wa kuwekeza katika utafiti lakini ni wajibu wa kila mmoja wetu ashiriki katika kuboresha huduma za afya. Tunataka dunia iwe sehemu nzuri ya kuishi. Ninaomba wadau wote wa sekta ya afya walioshiriki katika Kongamano hili la siku mbili mkafanye kazi kwenye maeneo yenu”,amesema.
Dk. Kapologwe ametumia fursa hiyo kuwapongeza na kuwashukuru waandaaji na washiriki wa kongamano hilo huku akibainisha kuwa serikali itayafanyia kazi mapendezo yaliyotolewa na wadau katika kuboresha sekta ya afya nchini.
Kwa upande wake, Meneja Mradi wa Asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) inayojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi Mkoa wa Mara Alio Hussen amesema AGPAHI inaendelea kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.
“AGPAHI kwa kushirikiana na Timu za Uendeshaji afya za mikoa, Halmashauri na Vituo vya kutolea huduma za tunatoa ya kuwajengea uwezo watoa huduma za afya ili waweze kutoa huduma bora ili kuhakikisha watoto wanazaliwa bila kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi lakini pia kuwahudumia watu wenye maambukizi ya VVU waendelee kuwa na nguvu na wafanye kazi kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya taifa letu”,amesema Alio.
Ameongeza kuwa AGPAHI ambayo sasa inafanya shughuli zake katika mkoa wa Shinyanga, Mara na Mwanza pia inashirikiana na serikali katika kuongeza nguvu kazi ‘wafanyakazi’ katika vituo vya afya,kuboresha miundombinu ya takwimu na mazingira ya kutolea huduma za afya na kusaidia katika upatikanaji wa dawa vifaa tiba na mfumo mzima wa ugavi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Kauli Mbiu ya Kongamano la Saba la Wadau wa Afya mwaka 2020 ni “Mafanikio ya Uchumi wa Kati Katika Kuweka Afya Bora kwa Watanzania – Transforming The Success of Middle – Income Economy Into a Healthier Nation)".
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa akifunga Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit) lililoshirikisha wadau wa sekta ya Afya kutoka taasisi za Umma, Mashirika ya dini na binafsi likiwemo shirika la AGPAHI leo Alhamis Novemba 26,2020 katika Ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa akifunga Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit).
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa akifunga Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit).
Washiriki wa kongamano la afya wakiwa ukumbini.
Wafanyakazi wa AGPAHI wakiwa kwenye Kongamano la Afya
Meneja Mradi wa AGPAHI mkoa wa Mara, Alio Hussein akizungumza kwenye Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit).
Afisa Mradi Usimamizi wa Ugavi wa Dawa AGPAHI mkoa wa Mwanza, Emilian Ng'wandu akitoa mada kuhusu ufanisi matumizi wa dawa mpya za ARV zenye Mchanganyiko wa Dolutegravir (DTG) na ushushwaji wa virusi kwa wateja waishio na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kama ilivyopendekezwa na UNAIDS kwenye kufikia 95-95-95 mara ifikapo mwaka 2030 Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit).
Afisa Mradi Usimamizi wa Ugavi wa Dawa AGPAHI mkoa wa Mwanza, Emilian Ng'wandu akiendelea kutoa mada kwenye Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit)
Afisa Mradi Usimamizi wa Ugavi wa Dawa AGPAHI mkoa wa Mwanza, Emilian Ng'wandu akitoa mada kwenye Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit).
Afisa Mradi - Usimamizi na Ugavi na Dawa AGPAHI mkoa wa Mara, Michael Bajile akitoa mada kuhusu mbinu mbadala zilizotumika kuhakikisha dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi zinapatikana kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (WAVIU) kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19. Alisema moja ya mbinu iliyofanikisha upatikanaji wa dawa hizo ni pamoja na kuongeza mawasiliano ya mara kwa mara na bohari ya dawa (MSD- Mwanza) na wadau wengine kuhakikisha kuna usafirishaji wa dawa kwa wakati. Pia uendeshaji wa mafunzo mbalimbali kwa watumishi wa afya kwa njia za kimtandao na kusaidia usambazaji wa dawa kati ya kituo na kituo pindi inapobainika upungufu au ukosefu katika kituo jirani (Reditributions).
Afisa Mradi - Usimamizi na Ugavi na Dawa AGPAHI mkoa wa Mara, Michael Bajile akitoa mada kuhusu mbinu mbadala zilizotumika kuhakikisha dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi zinapatikana kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (WAVIU) kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.
Afisa Mradi - Usimamizi na Ugavi na Dawa AGPAHI mkoa wa Mara, Michael Bajile akitoa mada kuhusu mbinu mbadala zilizotumika kuhakikisha dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi zinapatikana kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (WAVIU) kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kwenye Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit).
Afisa Mradi Mwandamizi Huduma za Kitabibu AGPAHI mkoa wa Mara , Dk. Faustine Kichah akitoa mada kuhusu mikakati inayofanywa na AGPAHI katika kukabiliana na changamoto ya Watu wanaoishi na maambuzi ya Virusi vya Ukimwi (WAVIU) kupotea kwenye huduma ya Tiba na Matunzo mkoani Mara kwa kupitia hospitali ya Kowak iliyopo wilayani Rorya.
Afisa Mradi Mwandamizi Huduma za Kitabibu AGPAHI mkoa wa Mara , Dk. Faustine Kichah akiendelea kutoa mada kwenye Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit).
Kiongozi na Msimamizi wa Mradi Ngazi ya Wilaya AGPAHI mkoa wa Mara, Jovin Jonathan akitoa mada kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika kuhakikisha watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI wanaendelea kupata huduma ya kupata dawa za kupunguza makali ya VVU(ARV) wakati wa janga la ugonjwa COVID 19 katika zahanati ya Makoko na Nyakato Manispaa ya Musoma Mjini.
Kiongozi na Msimamizi wa Mradi Ngazi ya Wilaya AGPAHI mkoa wa Mara, Jovin Jonathan akiendelea kutoa mada kwenye Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit).
Washiriki wa Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit) wakiwa ukumbini.
Washiriki wa Kongamano la 7 la Afya nchini (Tanzania Health Summit) wakiwa ukumbini.
Social Plugin