Marafiki wa milionea raia wa Zimbwabwe, Genius Kadungure aliyejulikana kama Ginimbi kwa muktadha wa kijamii, wamesema atazikwa na gunia lilojaa Dola, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Mfanyabiashara huyo aliyeishi maisha ya kifahari aliacha maagizo hayo kwa wanachama wa "all-white funeral", kama ilivyoandikwa na gazeti la Herald.
Ginimbi alifariki kutokana na ajali ya gari Jumapili, jijini Harare pamoja na mlimbwende Mitchelle Amuli aliyejulikana kama Moana.
Familia ya Moana imetaka fedha za mazishi kutoka kwa wanaowafariji.
Familia imeahirisha mazishi kwa wiki mbili ikisubiria majibu ya DNA na kukusanya michango ya kifedha kwa ajili ya kumuaga kwa heshima, imeripotiwa na Zim Morning post.
Matajiri wa Zimbabwe wamekuwa wakiahidi fedha kwa ajili ya mazishi ya Ginimbi.
Naibu Waziri Tino Machakaire ameahidi kununua jeneza kubwa kwa ajili ya Ginimbi, Mbunge Temba Mliswa amechangia wanyama wengi kwa ajili ya kuchinjwa kwenye mazishi hayo.
Wakati mwanasiasa Acie Lumumba ameahidi lita 1000 za mafuta ya dizeli, kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya ndani.
Ginimbi na Maona kwa pamoja walikuwa wanatoka kwenye sherere ya "all-white" ambapo gari yao iligongana na gari nyingine iliyokuwa inakuja mbele yao, ilichepuka nje ya barabara na kugonga mti kisha kulipuka moto.
Sherehe ya Ginimbi ya kuvalia mavazi meupe maarufu 'All White Party'
Ginimbi Genius Kadungure alijulikana kama mfalme wa mitindo mbali na kufanya sherehe kubwa .
Mwaka 2010 alifanya sherehe kubwa ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ambapo waliohudhuria walivaa mavazi meupe maarufu kama all White party mjini Harare Zimbabwe , sherehe hiyo ilizungumziwa sana mjini humo .
Miaka miwili baadaye mwaka 2012 alisimamia maadhimisho ya siku nyengine ya kuzalia kwake.
Mwaka 2013, Ginimbi aligharamia sherehe ya siku tatu katika kijiji cha kwao huko Domboshava ili kusherehekea nyumba mpya aliyojenga katika eneo hilo
Familia ya milionea maarufu nchini Zimbabwe, Ginimbi Genius Kadungure - aliyefariki na ajali ya gari Novemba 8, inasema watu watakaoudhuria mazishi ya milionea huyo siku ya Jumamosi lazima wavaa nguo nyeupe.
Mavazi hayo meupe yatavaliwa kama sawa na wakati alipokuwa hai, aliandaa sherehe na kutaka kila mmoja apendeze kwa kuvaa nguo nyeupe.
Vilevile alikuwa anawakumbusha mara nyingi kuwa hivyo ndivyo angependa kuzikwa , watu wasiwe na haraka haraka ya kumzika na wavae nguo nyeupe katika mazishi yake.
"Mchukue muda kupanga mazishi yangu. Nitahitaji kila anayehudhuria mazishi yangu avae nguo nyeupe tu, kupendeza ni lazima siku hiyo.
Tafadhali kumbuka kuchukua muda wenu muwezavyo kupanga mazishi yangu. Kumbuka ,nitakuwa nimevalia nyeupe tu. Hicho tu ndio ninakihitaji kwenye mazishi yangu." Juliet ambaye ni dada yake alinukuu maneno ya kaka yake alivyosisitiza kabla ya kifo chake.
Ginimbi Genius Kadungure, alifariki siku ya Jumapili , majira ya asubuhi katika mji wa Borrowdale, Harare, Zimbabwe.
Jina lake halisi ni Genius Kadungure na alikuwa maarufu kwa jina la Ginimbi.
Alizaliwa Oktoba 10,mwaka 1984. Hivyo amefariki akiwa na miaka 36.
Alikuwa mfanyabiashara maarufu , alikuwa mwenyekiti wa kampuni ya Piko Trading Holdings & Founder of Genius Foundation, na mmiliki wa klabu ya Sankayi (AKA Dreams Nightlife Club).
Alikuwa na 'Master of Business Administration - alipata MBA yake katika chuo kikuu cha at Great Zimbabwe.
Aliishi: Govan Mbeki, Mpumalanga, Afrika Kusini ingawa nyumbani ni Harare, Zimbabwe.
Moana mlimbwende aliyefariki katika ajali pamoja na Genius Kadungure
Mlimbwende huyu alikuwa maarufu Zimbabwe, alifariki akiwa kwenye gari moja na milionea Ginimbi Genius Kadungure.
Jina lake kamili ni Michelle Moana Amuli.
Ripoti zinasema kulikuwa na zaidi ya abiria mmoja na wote walifariki ndani ya gari lililopata ajali baada ya gari hilo kuwaka moto.
Kwa mujib wa ripoti ya polisi, Ginimbi, Moana na abiria wengine wawili walikuwa wametoka kwenye sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Moana aliyekuwa anatiiza miaka 26.
Kwa mujibu wa iHarere News, abiria wengine wawili ni Rolls Royce Wraith na Limumba Karim - mmoja akiwa raia wa Malawi na mwingine raia wa Msumbiji alifahamika kama 'Elisha'.
CHANZO - BBC
Social Plugin