Mgombea urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, amechukuliwa na polisi baada ya kuthibitishwa kuwa mgombea na tume ya uchaguzi, kulingana na mwandishi wa habari wa BBC Patience Atuhaire.
Alichukuliwa juu juu na polisi punde tu baada ya kumalizika kwa shughuli ya uteuzi wake na kupelekwa moja kwa moja hadi nyumbani kwake" Atuhaire amesema.
Wafuasi wa mwanasiasa huyo walikuwa wamekusanyika nje ya kituo cha uteuzi pamoja huku wengine wakiwa wanamsubiri barabarani.
Awali, polisi walikuwa wametangaza masharti makali juu ya idadi ya wafuasi wanaoruhusiwa kuandamana na mgombea urais hadi tume ya uchaguzi kuwasilisha stakabadhi zake.
Wafuasi wake waliokuwa wamekusanyika katika makao makuu ya chama chake cha National Unity Platform kwa ajili ya kuzinduliwa kwa manifesti yao walitawanywa kwa vitoa machozi.
Bobi Wine anakabiliana na wagombea wengine tisa kwenye kinyang’anyiro hicho akiwemo rais aliye madarakani Yoweri Museveni katika uchaguzi wa mwaka ujao.
CHANZO - BBC
Social Plugin