**********************************
Jamii imekumbushwa kuendelea kulinda haki za mtoto ikiwemo kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale kunapotokea uvunjifu wa haki zao.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na mshauri mwelekezi kwenye masuala ya haki za watoto na binadamu ambaye pia ni wakili Bi. Elida Kamaleki wakati akizungumza katika warsha iliyoratibiwa na Shirika la jukwa la utu wa mtoto CDF kwa kushirikiana na equality now, ambayo imezikutanisha asasi za kiraia 30 zinazofanya kazi na watoto ili kuweza kufahamu mifumo ya haki za binadamu ngazi ya kimataifa na kikanda.
Bi. Kamaleki amesema kuwa jamii lazima ijue kuwa inajukumu la kulinda haki za binadamu ikiwemo haki za mtoto kwa kufuatilia kama taarifa wanazotoa zinafanyiwa kazi ipasavyo
Naye Afisa Mawasiliano CDF,Bi.Celina Balagwiha amezitaka asasi hizo kujitafakari namna ya kubadilisha welekeo wao wa kufanya kazi ikiwemo kuwakutanisha watunga sheria na makundi yanaathirika na kuvunjiwa haki zao.
Mratibu mtendaji wa Asasi inayojihusisha kuelimisha jamii juu ya haki ya kina mama na Mtoto ili kutokomeza mila zenye madhara hasa kwa wanawake na watoto ya NAFGEM,Bw.Fransis Selasini amesema kuwa kukutana kwao kutakuwa msaada wa kutatua masuala ya haki za kibadamu kwa kuangalia kuanzia ngazi za kitaifa mpka kimataifa.