Picha : DC NYAMAGANA AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA...AWAHIMIZA KUTUMIA MAFUNZO KWA MANUFAA YA TAIFA

Mkuu wa Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza, Dkt. Philis Nyimbi amefunga mafunzo ya awali ya askari wa jeshi la akiba (mgambo) wilayani humo na kuwahimiza wahitimu wa mafunzo hayo kuyatumia vyema kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Dkt. Nyimbi amefunga mafunzo hayo Jumatano Novemba 11, 2020 katika uwanja wa Shule ya Msingi Iseni Kata ya Butimba jijini Mwanza na kueleza kwamba Serikali inatambua na kuthamini mchango wa askari wa jeshi la akiba hususani katika kushirikiana na vyombo vingine vya dola katika kuimarisha ulinzi na usalama katika jamii.

Naye Mshauri wa Mgambo Wilaya Nyamagana, Meja Prisca Ishanju alibainisha kuwa jumla ya askari 85 wamehitimu mafunzo hayo ya awali ya jeshi la akiba yaliyoanza Agosti 08, 2020 ambapo askari wa kiume ni 70 na wa kike wakiwa ni 15 huku wawili wakishindwa kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo za kiafya.

Nao askari waliohitimu mafunzo hayo kupitia risala iliyosomwa na Prepetua Stephano wameiomba Serikali kuwapatiwa mafunzo ya awali ya pili ili kujiimarisha zaidi huku wakiongeza kuwa mafunzo waliyoyapata pia yatawasaidia kujiajiri na hivyo kuomba kunufaika na fedha za asilimia 10 zinazotolewa na Halmashauri nchini ili kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akizungumza kwenye kilele cha mafunzo ya askari wa jeshi la akiba wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akizungumza kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mshauri wa Mgambo wa Wilaya Nyamagana, Meja Prisca Ishanju.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya awali kwa askari wa jeshi la akiba wilayani Nyamagana, Prepetua Stephano (kushoto) akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake. Kulia ni Zena Issa mmoja wa wahitimu hao.
Risala ya wahitimu kwa mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akipokea risala ya wahitimu.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (kushoto) pamoja na Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya Nyamagana, Meja Prisca Ishanju (kulia).
Wahitimu wa mafunzo ya awali ya jeshi la akiba wilayani Nyamagana wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi kukagua gwaride.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya awali ya jeshi la akiba wilayani humo.

Askari wa jeshi la akiba wilayani Nyamagana wakionyesha ukakamavu mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (hayuko pichani).
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (wa nne waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na askari wahitimu wa mafunzo ya awali wilayani Nyamagana na viongozi mbalimbali wilayani humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post