Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua gwaride la Jeshi la akiba.
Na Marco Maduhu - Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amehitimisha rasmi mafunzo ya Jeshi la akiba kwa vijana 138 kutoka manispaa ya Shinyanga.
Hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo imefanyika leo katika viwanja vya mtaa wa Mabambasi Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga, na kuhudhuriwa pia na wananchi.
Akizungumza, Mboneko amewataka vijana hao waliohitimu mafunzo ya Jeshi la akiba, wakawe chachu ya kudumisha amani ndani ya jamii, na wasiwe chanzo cha kuvuruga amani na kuanza kupiga watu hovyo.
"Nyie mmeshaiva mara baada ya kupata mafunzo ya Jeshi la akiba, na kuwa askari kamili, hivyo mkirudi mitaani msiwe chanzo cha uvunjifu wa amani, bali mkawe walinzi wa amani," amesema Mboneko.
Pia amewataka wajiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali, ili wapate fedha za halmashauri na kufanya biashara mbalimbali, ambazo zitawainua kiuchumi, na kuacha kujiingiza kwenye vikundi vya uharifu, sababu wameshapata mafunzo ya kijeshi.
Naye mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la akiba Ezra Majerenga,akisoma risala, alisema wamehitimu 138, wavulana 114, na wasichana 24.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa kufunga rasmi mafunzo ya Jeshi la akiba.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akionya vijana hao waliohitimu mafunzo ya Jeshi la akiba kuepuka kwenda kufanya fujo mitaani na kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.
Mshauri wa Jeshi la akiba wilaya ya Shinyanga Ford Mwakasege, akisoma taarifa ya mafunzo hayo ya Jeshi la akiba.
Mhitimu wa mafunzo ya Jeshi la akiba Ezra Majerenga akisoma risala kwa niaba ya wenzake.
Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Shinyanga ikiwa kwenye kuhitimisha mafunzo ya Jeshi la akiba.
Wananchi wakishuhudia ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la akiba.
Wananchi wakishuhudia ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la akiba.
Vijana waliohitimu mafunzo ya jeshi la akiba wakisiliza nasaha kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu jeshi la akiba, wakicheza gwaride.
Wahitimu Jeshi la akiba wakiwa kwenye Gwaride.
Wahitimu Jeshi la akiba akila kiapo cha utii.
Wahitimu Jeshi la akiba akifurahia mara baada ya kuhitimu mafunzo yao.
Burudani zikitolewa.
Burudani zikiendelea kutolewa.
Burudani zikiendelea kutolewa.
Burudani zikiendelea kutolewa.
Wahitimu waliofanya vizuri wakipewa zawadi.
Wahitimu waliofanya vizuri wakipewa zawadi.
Wahitimu waliofanya vizuri wakipewa zawadi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (Katikati)akipiga picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wilaya, na wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la akiba.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.