Diwani mteule wa kata ya Kinuni iliyopo Zanzibar, Suleiman Mohamed Hassan (CCM) amefariki dunia.
Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM kwa upande wa Zanzibar, Catherine Peter Nao amesema diwani huyo alifariki ghafla juzi baada ya kuanguka nyumbani kwake na kupelekwa katika Hospitali ya Altabib.
Hassan alifariki dunia muda mfupi baadaye akiwa katika hospitali hiyo.
“Sisi kama CCM tumepokea kwa masikitiko taarifa ya msiba wa diwani Hassan na tunaiomba familia yake kuwa na moyo wa subira,” amesema Nao.
Via Mwananchi
Social Plugin