Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, hafla hiyo ya kukabidhiwa Cheti imefanyika katika Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 01 Novemba 2020.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Makamu wa Rais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kiongozi wa Jopo la Waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020 Rais Mstaafu wa Burundi Silvestre Ntibantunganya mara baada ya kukabidhiwa Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage leo tarehe 01 Novemba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Waliogombea Urais kupitia vyama Mbalimbali vya Upinzani nchini wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa katika hafla fupi ya kukabidhi Cheti cha Ushindi kwa Kiti cha Urais zilizofanyika katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 01 Novemba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mara baada ya kukabidhiwa Cheti cha Ushindi kwa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wageni mbalimbali waliofika katika hafla fupi ya kukabidhiwa Cheti cha Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Social Plugin