Mwanaume mmoja mkazi wa Baringo nchini Kenya ambaye alikuwa amekamatwa na polisi kwa kuiba mbuzi na sungura kutoka nyumbani kwa mpenzi wake kama njia ya kujilipa fidia pesa 'nauli' alizompa mrembo halafu hakwenda kwake ameachiliwa huru baada ya familia ya mrembo huyo kuamua kutanzua kesi hiyo nje ya mahakama.
Daniel Kemboi, 27, alivamia boma la familia ya Kipchere na kuondoka na wanyama hao kama njia ya kujilipa fidia ya KSh 1,500 ambazo alidai alimtumia Vivian Jebet (24), mara kadhaa kama nauli ya kwenda kwake.
Kwa mujibu wa taarifa ya K24, jamaa huyo ambaye anaishi katika kijiji cha Koroto, Kaskazini mwa Baringo alisema Jebet alimung'unya pesa hizo na kuacha kufika kwake kama walivyokuwa wamekubaliana hivyo jamaa akavamia makazi ya mrembo huyo na kuiba mbuzi na sungura kama njia ya kujilipa fidia pesa ambazo alimtumia mrembo huyo.
Kemboi alikamatwa kwa kuchukua mifugo hiyo baada ya baba mzazi wa Jebet kumshtaki kwa polisi
Mshukiwa huyo alikuwa anatazamiwa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kabarnet jana Jumatatu, Novemba 2, lakini familia ya mrembo iliamua kutatua kesi hiyo nje ya korti.
Hivi karibuni pia mwanamke mmoja mjini Kisumu ambaye alikuwa ameingiwa na hofu baada ya mpenzi wake wa zamani kutishia kumtumia polisi.
Mwanamke huyo ambaye ni shabiki sugu wa mwanablogu Edgar Obare, alisimulia kuwa alimuagiza mpenzi wake amtumie nauli ya KSh 2,000 ili aende kumtembelea lakini alitumia pesa hizo na kukosa kwenda.
Jambo hilo lilimkera sana jamaa huyo ambaye alipiga ripoti kwa polisi.
Mtindo huo wa wanawake kuwahadaa wanaume kuwatumia nauli umekuwa ukiwadunisha wanaume wengi.
Aoko Otieno hii majuzi aliwashambulia wanawake wenye hulka hizo na kuwataja kama wezi.
Aoko alisema wanaume hutuma pesa hizo wakiwa na sababu zao na hivyo kuwataka wanawake wajiwasilishe baada ya kupokea pesa hizo.
CHANZO - TUKO NEWS
Social Plugin